June 4, 2019


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga kwa sasa upo kwenye mazungumzo na winga wa kikosi cha Tanzania Prisons, Ismail Azizi kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao.

Yanga kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao na tayari wameanza kusainisha wachezaji wapya ambao wataifanya timu hiyo kuleta ushindani.

Azizi amesema kuwa amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa Yanga hivyo mambo yakijipa huenda atabadilisha jezi na kuwa ndani ya uzi wa njano msimu ujao.

" Wengine ni Adam Koseja ambaye ni mlinda mlango, Jukumu Kibanda yeye ni beki, Daniel Joram, Seleman Bwenzi na Lusajo Leliarant mwenye mabao 16 hawa ni washambuliaji pamoja na Jamal Duraz pamoja na John Kelvin ambaye ni kiungo hawa walikuwa na timu awali wamepewa kandarasi ya miaka miwili," alisema Namlia.

"Viongozi wa Yanga wamenifuata na tumezungumza mambo mengi kuhusu kujiunga kwao ila mpaka sasa bado hatujafikia muafaka wowote endapo mambo yatakamilika huenda msimu ujao nitakuwa ndani ya kikosi chao, ila ninawashukuru sana Tanzania Prisons kwa kunipa nafasi ndani ya kikosi," amesema.

Uongozi wa Yanga, kupitia kwa Makamu Mwenyekiti, Frederick Mwakalebela amesema kuwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameacha ripoti na orodha ya wachezaji ambao wanatakiwa kusajiliwa hivyo mchakato bado unaendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic