July 7, 2019


BAADA ya timu ya Taifa ya Misri kutolewa hatua ya 16 bora na timu ya Afrika Kusini kwa kufungwa bao 1-0 jana uwanja wa Taifa wa Cairo, imeripotiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Misri, Hany Abourida amemtimua kocha Mkuu Javier Aguirre.

Aguirre alikuwa na kandarasi ya miaka minne ndani ya kikosi cha Mapharaoh hao na alikuwa analipwa dola 120,000 kwa mwezi, pia imeripotiwa kwamba baada ya kutoa adhabu hiyo Rais huyo amejiuzulu nafasi yake pamoja na makamu wake naye Ahmed Shobeir naye amejiuzulu.

7 COMMENTS:

  1. Ukisikia kuwajibika ndio huko sio kuwalaumu wachezaji tu.

    ReplyDelete
  2. Mfano wa kuigwa. TFF mnajifunza nini hapo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hehee waachie ngazi? Si uliwasikia wanatuambia tusimsakame kocha

      Delete
  3. Ni vizuri kama wameachia nafasi ili na wengine washike nafasi kwa kupeleka mbele gurudumu hilo.

    ReplyDelete
  4. Ni mfano wa kuigwa, sio nyie tff ya kibongo eti mnamtimua kocha pekee yake inatakiwa na nyie mjiudhulu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic