MAMBO yanazidi kupamba moto kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza Agosti 23 ambapo kikosi cha Yanga kimejipanga kuleta ushindani wa kutosha.
Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao pamoja na michezo ya michuano ya kimataifa.
Miongoni mwa nafasi ambazo zinatajwa kuwa na ushindani mkubwa wa namba ni pamoja na viungo wa timu ambapo mpaka sasa wapo wachezaji 10 ambao wanafiti nafasi hiyo.
Viungo hao ni pamoja na Pappy Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Mo Banka, Mapinduzi Balama, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Deus Kaseke, Fei Toto, Abdulaziz Makame na Said Juma Makapu.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa sababu kubwa ya kusajili wachezaji wengi ni kuleta ushindani mkubwa.
"Malengo yetu ni kuona tunakuwa na kikosi chenye ushindani msimu ujao, kila mchezaji ana shauku ya kuonyesha uwezo wake," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment