July 6, 2019


BAADA ya kuzuka ghafla kwa taarifa kuwa ndani ya uongozi wa Klabu ya Simba hakuna maelewano huku ikidaiwa mwekezaji klabuni hapo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwa mbioni kung’atuka, Crescentius Magori amefunguka kila kitu.

Taarifa za Mo kutaka kuondoka Simba zilianza kusambaa mitandaoni kuanzia Alhamisi lakini hakukuwa na kiongozi yeyote wa timu hiyo aliyeitisha mkutano wa wanahabari kwa ajili ya kuweka wazi nini kinaendelea.

Kitendo cha Mo Dewji kuandika ‘caption’ za mafumbo kwenye mitandao yake ya kijamii, kilizidi kuwavuruga wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imetwaa ubingwa wa ligi kuu mara mbili mfululizo.

Championi Jumamosi, lilifanikiwa kuzungumza na Magori ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kuhusiana na ishu hiyo ambapo alisema, kwa sasa hakuna tatizo lolote ndani ya timu hiyo na kwamba kila kitu kinakwenda sawa kama walivyopanga.

“Hakuna mgogoro wowote ndani ya Simba, kwa sasa kila kitu kinakwenda kama ambavyo kimepangwa, mashabiki wa Simba wanapaswa watulie wasifuate taarifa ambazo hazina ukweli,” alisema Magori.

Naye Mwenyekiti wa Simba, Suedy Mkwabi alisema: “Kwa sasa nipo nchini China, nashughulikia masuala ya biashara zangu, hivyo masuala ya migogoro ndani ya Simba mimi sifahamu, najua kwamba kila kitu kipo sawa.”

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mo Dewji, jana aliandika kwamba: “Kwenye uongozi na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayehujumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao.”

3 COMMENTS:

  1. Ukiangalia utaona hakuna shaka yeyote kuwa Mo Dewji yapo serious katika kuibadilisha Simba kuwa klabu ya maana katika ukanda wetu huu.Mo sio malaika lazima kutakuwa kuna vitu vinamfurahisha na kumchukiza. Kueleza hisia zake kama binaadamu kwa jinsi anavyoona mambo yanavyoenda ndani ya taasisi anayoiongoza kwanini watu wanachukulia katika msimamo ghasi zaidi kama vile Mo anataka kuibomoa Simba ilhali nia yake kubwa ni kutaka kuona mambo yanakwenda vizuri zaidi ya sasa pale simba. Hata Magufuli ameshatimua viongozi wangapi alioona wanamkwamisha kufikia malengo yake. Kweli Kuna wanaopinga mabadiliko ndani ya Simba na inawezekana kabisa kuna wanaopinga kujiopandikiza au kupandikizwa ndani ya uongozi wa Simba wa sasa ila tuwe wawazi bila ya uoga wowote wa kutambua mafanikio na kuyasemea bila kigugumizi kuwa mafanikio ya Simba ni ingizo jipya katika mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano na kama kutatokea kufeli uwekezaji ndani ya klabu ya Simba basi taasisi husika ya serikali haikwepi kuhusika na lawama.
    Kumeibuka aina fulani ya siasa hivi ndani ya vilabu vyetu hasa Simba na Yanga na kana kwamba wanasiasa anaonekana kuegemea klabu fulani hivi licha ya klabu husika kuwa na mfumo uliofeli lakini wakipigiwa debe kama vile ni klabu yenye mafanikio. Fitina za chuki za kubomoa za baadhi ya wanasiasa labda kwa utashi wao na mapenzi yao na klabu yao kwa kutumia nguvu zao za kisiasa wameamua kupeleka hujuma ndani ya Simba na Mlengwa mkuu wanaemlenga ni Mo Dewji. Wanajua ili kuimaliza Simba within second basi ni kumvuruga Mo. Na kama ujumbe wangu huu utafika kwa Mohammed Dewji ni kwamba wanasimba wapo pamoja nae kwa shida na kwa ziki.Asiwaache asilani tu hivi hivi kwa tatizo sijui la mwenyekiti wa klabu litapita hilo na ikiwezekana atafute usuluhisho you're smart enough solving tough issue more than that. Nasema Mo asiawaache wanasimba kwa ukorofi wa wachache kwa sababu nakumbuka wakati Mo alipotekwa jinsi gani wanasimba nchi nzima walivyokuwa wanapambana kutafuta ufumbuzi wa kumuokoa yeye na maisha yake. Mpaka vyombo vya Dola vikawa vinahofu kutokea kwa machafuko makubwa ya uvunjifu wa amani katoka kwa wanachama na wapenzi wenye hasira wa Simba kutoka kwenye kila kona ya nchi hii hadi kupelekea kuwekwa ndani kwa siku kadhaa kwa msemaji na muhamasisaji mkuu wa Simba khaji Manara. Wanasimba walifanya yote ili Mo apatikane,walisali,
    walisoma halibadri,walitoa sadaka katika nyumba za ibada na kwa watoto yatima,Walifunga kumuomba M/Mungu ili mo apatikane na walikuwa wapo tayari kuingia mitaani na msituni kupekua Nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba,dari kwa dari,choo kwa choo,msitu kwa msitu,kichaka kwa kichaka,gari kwa gari,bus kwa bus nakadhalika mpaka kieleweke. Utaona hapo kiasi gani watu wa Simba wanavyothamini mchango wa Mo ndani ya timu yao na kuwa na mapenzi yao binafsi juu yake achana na utajiri wake bali Mo ni Mtu wa watu. Wanasimba moja ya kitu wanachojivunia ni kubahatika kuwa na mtu kama Mo Dewji kwenye familia ya Simba. Mo ni moja ya hazina muhimu ndani ya klabu ya Simba na hazina huwa haiondoki wala kuchezewa kirahisi rahisi. Ningemuomba tu Mr Magori na ni moja ya beautiful people that simba have right now, kuelekea simba day kuwe na wiki maalum ya Mo week ili kuonesha thamani ya mchango wake ndani ya simba na maendeleo yake.

    ReplyDelete
  2. Ni vyema vilabu za kibongo kutafuta mbinu nyingine kujitegemea pasipo kuwategemea wafadhili.

    ReplyDelete
  3. Hata nchi zina wafadhili ili mambo yaende.Tatizo sio ufadhili bali tatizo ni watanzania kutojielewa. Suala la Simba lilishapatiwa ufumbuzi kwa wanachama kuamua kwa kauli moja kwamba timu yao itajiendesha kwa mfumo wa hisa na hakuna kurudi nyuma sasa kuna wapumbavu fulani wanajaribu kukwamisha maamuzi ya wanachama wa Simba na watu wanawachekea kwanini Mo asifikirie kuchukua uamuzi unaofaa? Wanachama wa Simba wakiona hakuna kinachofanyika cha maana ndani ya simba wanajua ni Mo ndie anaewachelewesha kumbe kuna wasaliti ndio wanaofanya hujuma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic