July 7, 2019


RAIS wa TP Mazembe, Moise Katumbi ameruka tuhuma za gazeti moja la Madagascar kwamba alimhonga kipa wa Zimbabwe kwenye mechi ya Afcon kuwania kufuzu 16 Bora dhidi ya DR Congo.

DR Congo ya Mwinyi Zahera ilishinda mabao 4-0 kwenye mchezo huo na kufuzu jambo ambalo liliibua mijadala mingi.

Habari zilimhusisha Katumbi na kipa wa Zimbabwe kwamba amempa mshiko ili alegeze jambo ambalo amelikana na tayari amepeleka utetezi wake Caf.

Kupitia ujumbe wake kwenye Twitter yake, Katumbi amesisitiza madai hayo ni ya hovyo na kwamba hata siku mechi hiyo inachezwa hakuwepo Misri alisharudi zake Congo.

Kiongozi huyo mwenye heshima kwenye soka la Afrika amesisitiza kwamba hawezi kuhusika kwenye mambo ya hovyo kama hayo ya kupanga matokeo. Huku uchunguzi ukiendelea, DR Congo itacheza na Madagascar leo Jumapili kwenye mechi ya 16 Bora

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic