WACONGO WAMUONDOA ULIMWENGU KWA WAARABU
Imeeleza kuwa Klabu ya aS Vita ya Dr Congo imekomaa na mpango wake wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa JS Saoura ya algeria, Thomas Ulimwengu kwa ajili ya msimu ujao.
Saoura ilimsajili Ulimwengu hivi karibuni akitokea katika Klabu ya Al Hilal ya Sudan ambapo awali alikuwa nje kutokana na kuandamwa na majeraha kwa muda mrefu.
Taarifa zinadai kuwa licha ya Vita kukomaa na suala la kutaka kumsajili nyota huyo lakini ngoma imekuwa ngumu kwa wao Saoura ambao wameonekana wazi bado wana mpango wa muda mrefu na nyota huyo.
Ulimwengu tangu asajiliwe kikosini humo, amekuwa hana nafasi sana kama ambavyo ilikuwa kwa timu zake za awali za TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan ambako alicheza kwa muda mfupi.
Championi Jumamosi lilifanya mawasiliano na wakala wa mchezaji huyo, Ibrahim Camara naye aliweza kufunguka: “Ni kweli AS Vita wanapambana kumpata Thomas Ulimwengu lakini sina hakika kama JS Saoura watakuwa tayari kuweza kumuachia, ngoja tusubiri.”
0 COMMENTS:
Post a Comment