TIMU yetu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kucheza mchezo wake wa kimataifa
ambao ni maalumu kwa kufunzu michuano ya Chan Agosti 28 dhidi ya Kenya.
Ni muda wa
wachezaji wetu wa timu ya Taifa kuipeperusha vema Bendera ya Taifa kwa
kupambana na kupata matokeo chanya.
Tukumbuke
kuwa tunaanza kucheza nyumbani hivyo kipaumbele kikubwa iwe ni kupata matokeo
chanya kwenye mchezo wa kwanza.
Ushindani ni
jambo la lazima na Kenya ni jirani zetu tumekuwa na historia ya kupata
ushindani mkubwa kwao sasa ni lazima huo mwiko tuuvunje.
Tusisahau
kwamba walitufunga mabao 3-2 tulipocheza nao kwenye michuano ya Afcon nchini
Misri sasa wanakuja kwetu tujipange.
Kila timu
inatafuta nafasi nasi pia tunapaswa tuonyeshe kwamba tunaweza na hatubahatishi
tukiwa nyumbani.
Kila la
kheri timu yangu ya Taifa na wachezaji wote mnapaswa mjitume kwa hali na mali
kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo.
Tukiachana
na Stars acha tuje huku kwenye Ligi Kuu Bara ambapo tunaona tayari maandalizi
ya msimu ujao yameanza kupamba moto.
Baada ya
ratiba kutoka ambapo inaonesha kwamba Agosti 23 Ligi Kuu Tanzania Bara inaanza
kutimua vumbi ni muda mwafaka kwa kila timu kujipanga vema.
Maandalizi
ya awali ni muhimu kwa kuwa ndiyo yanatengeneza picha ya timu kamili
itakayopambana msimu ujao na kuleta mafanikio ambayo yanahitajika.
Mipango
sahihi ni lazima kwa sasa ipangwe hasa kwa zile timu ambazo msimu ulipita
zilikuwepo kwenye ligi na ziliona namna hali ilivyokuwa ya kusuasua hasa kwa
upande wa fedha.
Pia
ikumbukwe kwamba zipo ambazo ziliponea chupuchupu kushuka daraja ni jambo la
kuzingatia kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza.
Kama
hakutakuwa na mipango makini tusitarajie ushindani mkubwa kutoka kwa zile timu
ambazo hazijajiandaa ni muda mwafaka wa kufanya mambo makubwa hasa kwa kuanza
maandalizi mapema.
Kila timu
ipange mkakati wake mapema na kuwapa wachezaji ambao tayari wameshasajiliwa na
timu zote kwa ajili ya matumizi ya msimu ujao.
Inasikitisha
pia inaumiza kuona kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya timu hazijafanya usajili wa
aina yoyote zaidi zenyewe zinazidi kubomolewa kwa wachezaji wao kuchukuliwa na
timu nyingine hii ni mbaya kwa sasa.
Nasema ni
mbaya kwa kuwa ukweli ni kwamba dirisha la usajili linakaribia kufungwa na
likifungwa hakutakuwa na muda mwingine wa kusajili sasa unafikiri wachezaji gani
watakaoitumikia timu ilihali hakuna usajili?
Haina maana
ama ulazima kwamba kwenye kila dirisha
la usajili lazima timu isajili hapana inategemea na ripoti ya mwalimu lakini
cha msingi ni kuangalia ni wachezaji wangapi wenye uzoefu ambao timu imewaacha
wajiunge na timu nyingine? Je wale ambao wapo wataweza kuleta ushindani ?
Kama maswali
haya yakipata majibu na uongozi wa timu ukakubali kwamba hakuna ulazima wa
usajili na wanawaamini wachezaji waliobaki hakuna shida mambo acha yaendelee
ila ninachoamini kwamba kwa vyovyote vile usajili ni kitu cha muhimu hasa
kuelekea msimu mpya.
Timu nyingi
zilikwama msimu uliopita kutokana na kufanya usajili usiokidhi vigezo wachezaji
wengi walikuja kuonyesha kwamba hawawezi kuleta ushindani hivyo ni somo jingine
kwamba usajili ni lazima uwe ule uliofanyiwa uchunguzi.
Timu nyingi
zinafeli kwenye scout ya wachezaji jambo ambalo linawafanya waishie kutazama
video kwenye mitadao kisha wanajidanganya kwamba mchezaji mzuri sio kweli.
Kwa zama
ambazo tupo kwa sasa ni lazima klabu zote ziamke ziwe zinafuatilia michuano ya
ndani zitapata vipaji vya kweli.
Wakati
mwingine timu zinasajili wachezaji kutoka mataifa ya mbali ilihali hata ndani
wapo wenye uwezo zaidi ya hao wanaosajiliwa tatizo ni kwamba hakuna ambaye
anawafuatilia kwa ukaribu na kujua ni nani anayestahili kucheza ndani ya klabu
kwa wakati huo.
Umakini
katika kila jambo unahitajika ili kupata matokeo chanya msimu ujao, tunahitaji
kuona ushindani unaongezeka na kwa timu zote.
0 COMMENTS:
Post a Comment