LIONEL Messi mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Argentina amesema kuwa hana imani na waandaaji wa michuano ya Copa America kwani wanawapendelea waandaaji ambao ni Brazil.
Messi alionyeshwa kadi nyekundu kwenye michuano hiyo dakika ya 37 na kumfanya afikishe jumla ya kadi mbili nyekundu akiwa na timu ya Taifa baada ya kusuguana na mchezaji wa Chile Gary Medel kwenye michuano ya Copa America.
Kadi yake ya kwanza Messi aliipata mwaka 2005 akiitumikia timu ya Taifa na ilikuwa mechi dhidi ya Hungary.
Licha ya Messi kunyoosha mikono yake juu haikumzuia refa wa mchezo huo, Mario Diaz de Vivar kuwaonyesha kadi nyekundu wachezaji hao.
Messi amesema kuwa hana imani na waandaaji wa michuano ya Copa America kwani wameyafanya yawe maalumu kwa ajili ya waandaaji wa michuano hiyo ambao ni wabrazil.
Licha ya kutolewa kwa Messi walishinda kwa mabao 2-1 na aligoma kurejea kuvaa medali za ushindi wa pili.
Mshindi wapi vipi wakati argentina walitolewa nusu final?
ReplyDelete