July 9, 2019


KOCHA msaidizi wa timu ya Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wamepoteza mchezo wa leo kutokana na mchanganyiko wa wachezaji wapya na wazamani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa haina tatizo kupoteza mchezo wa leo mbele ya KCCA kwa kufungwa bao 1-0 kwani ni sehemu ya mchezo.

"Tumepambana ila haikuwa bahati yetu kwani wachezaji wetu bado wana mchanganyiko kuna wale wapya na wazamani hivyo muda si mrefu tutakuwa bora, mchezo wetu unaofuata tutapambana kushinda," amesema.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame wanaiwakilisha Tanzania wakiwa na KMC, mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 mbele ya Mukura FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic