MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' Simon Msuva amesema kuwa leo watapambana kufanya vema kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria.
Stars haijawa na matokeo chanya kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri baada ya kupoteza michezo yote miwili waliyocheza hatua ya makundi na leo watamenyana na Algeria.
"Tulipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal, tuliumia, tukapoteza pia mbele ya Kenya tuliumia zaidi ila kwa sasa tumejifunza kupitia makosa ni zamu yetu kufanya vizuri na tuna imani ya kufanya vizuri," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment