July 31, 2019


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ni busara kwa uongozi wa Yanga kumalizana na wachezaji wake wote wa zamani wanaowadai kabla ya kumalizana na wachezaji wapya.

Inaelezwa kuwa Yanga imewasimamisha wachezaji wake watatu ambao wanawadai stahki zao ambao ni Juma Abdul, Andrew Vincent 'Dante' na Kelvin Yondani.

Zahera amesema:"Wachezaji wote waliongea na mimi ikiwa ni pamoja na Abdul pamoja na Dante, waliniambia kwamba wanadai stahiki zao kwa muda mrefu na hawajapewa hata shilingi, hivyo nilichowashauri ni kwamba wawe na subira.

"Isitoshe hawa wachezaji wa zamani ni miongoni mwa walioleta wazo la kuichangia timu ili ipunguze gharama za uendeshaji hivyo wana haki ya kuwa ndani ya timu na kulipwa kwa kupunguziwa yale madeni kuliko kuanza kuwekeza kwa wachezaji wapya.

"Busara kugawana hasa baada ya kupata fedha, hivyo kama kutakuwa na elfu moja ni vizuri kuwapa hata mia nane huku tukiendelea kupambana na mambo mengine,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic