July 5, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesikia taarifa za beki wake wa pembeni, Gadiel Michael kugomea kusaini mkataba akasonya na kuwaambia viongozi; “Mnambembeleza wa nini?”

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu mmoja wa viongozi wa Yanga kusafiri na mkataba hadi nchini Misri inapofanyika Afcon kwa ajili ya kumsajili beki huyo aliyekuwa Taifa Stars iliyoondolewa katika michuano hiyo.

Beki huyo kwa mara ya pili amegomea kusaini mkataba baada ya hivi karibuni kukataa dau la Shilingi Milioni 50 alilowekewa mezani huku Simba ikielezwa kumuwekea 70 ambazo ameshawishika kusaini miaka mitatu Msimbazi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Zahera tayari amewaambia mabosi wa timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kwavile si staa kiasi hicho wala gharama yake si kubwa kiivyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kocha huyo tayari ametoa mapendekezo ya kumbakisha Haji Mwinyi aliyekuwa kwenye mipango ya kuachwa kwa ajili ya kusaidiana na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Aliongeza kuwa, kocha anaamini kuwa wapo wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi ya Gadiel, hivyo kuondoka kwake hakutamuumiza huku akimtakia kila heri huko aendako.

Habari zinasema Mwenyekiti wa timu hiyo, Mshindo Msolla ametoa mpaka kufikia leo Gadier kuelezea hatma yake kusaini Yanga kabla ya wao uongozi kufanya uamuzi.

7 COMMENTS:

  1. Gadieli Michael ni mbovu sana kwenye kukaba magoli mengi ya Timu ya Taifa na hata mechi za ligi kuu yalikuwa yanapitia upande wake fuatilia mechi za Taifa Stars na za Yanga utakubaliana namimi....Kama mimi ndio nasajili Simba natafuta namba 3 ni mara mia nimchukue Godfrey Walusimbi kuliko Gadieli Michael....yeye (Gadieli) ni mzuri tu kwenye kushambulia....kitu ambacho Mohamed Husein Tshabalala anacho na zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Gadiel ni mzuri kuliko Tshabalala. Tshabalala hajui kukaba but Gadiel no mwepesi na alikuwa na uwezo wa kurudi kuja kusaidia nyuma.

      Delete
  2. Hawa vijana wamedanganywa na washauri wabovu walionao kwa kudhani kuwa wana viwango vya juu ama kutafuta pesa nyingi kwa ajili ya maisha lakini wanashindwa kujua kuna siku utafilisika na pesa uliyopewa itaisha na itabidi utafute nyingine wakati huo kiwango kimeshuka hamna mtu aliye tayari kukusajili....na kwakuwa umri ni mdogo hata nje hawawezi kukuchukua ikiwa nidhamu yako n.a. kiwango chako kimeshuka.....pesa ni muhimu lakini sio kila kitu....wachezaji wetu inatakiwa wapewe somo la kujitambua ama sivyo wataishia humu humu kukata mitaa ya kariakoo

    ReplyDelete
  3. Hawa vijana wamedanganywa na washauri wabovu walionao kwa kudhani kuwa wana viwango vya juu ama kutafuta pesa nyingi kwa ajili ya maisha lakini wanashindwa kujua kuna siku utafilisika na pesa uliyopewa itaisha na itabidi utafute nyingine wakati huo kiwango kimeshuka hamna mtu aliye tayari kukusajili....na kwakuwa umri ni mdogo hata nje hawawezi kukuchukua ikiwa nidhamu yako na kiwango chako kimeshuka.....pesa ni muhimu lakini sio kila kitu....wachezaji wetu inatakiwa wapewe somo la kujitambua na uweledi, na namna ya kufikiria future yao zaidi katika kukuza na kuviendeleza vipaji vyao, ama sivyo wataishia humu humu kukata mitaa ya kariakoo

    ReplyDelete
  4. We ujaona tshabalala alivoruhusu goli mbili dhidi ya Algeria gadiel mzuri

    ReplyDelete
  5. Alipo igomea Azam na kujiunga na Yanga olikuwa sawa tu leo anaigomea Yanga inaonekana tatizo. Alligomea Azam kwa sababu ya Maslahi na anaigomea ya kwa sababu ileile au kwa Simba na Yanga wachezaji hawana haki?

    ReplyDelete
  6. Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic