July 5, 2019


Beki wa klabu ya Yanga, Gadiel Michael amesema yupo tayari kusaini Yanga mkataba mpya iwapo tu klabu hiyo itafikia dau na masharti ambayo amewapa, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Gadiel amedai mpira ndiyo kazi yake hivyo amewapa mapendekezo viongozi wa klabu ya Yanga ili kusaini mkataba mpya.

Gadiel amefunguka kwa kusema kuwa, iwapo watashindwa mpaka tarehe 06 July atasaini klabu nyingine ambayo imekubali kumpa dau alilolitaka.

Tetesi za ndani zinasema tayari mchezaji huyo amefikia makubaliano na Simba ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

19 COMMENTS:

  1. Nyie yanga hebu muacheni jamaani,mbona mnabembeleza Sana?

    ReplyDelete
  2. Nyie yanga hebu muacheni jamaani,mbona mnabembeleza Sana?

    ReplyDelete
  3. Simba wamsaini tu bwana mdogo anaonekana anaipenda kazi yake na Simba panamuhusu ili kuongeza uwezo wake na ushindani zaidi .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini hata huyo Gadieli hamna kitu tuseme ule ukweli tu....magoli mengi hutokea kwake....Yanga mna bahati sana kwakuwa sasa mtaziba moja ya mapungufu ya beki mliyokuwa nayo msimu uliopita

      Delete
  4. Gadieli Michael ni mbovu sana kwenye kukaba magoli mengi ya Timu ya Taifa na hata mechi za ligi kuu yalikuwa yanapitia upande wake fuatilia mechi za Taifa Stars na za Yanga utakubaliana namimi....Kama mimi ndio nasajili Simba natafuta namba 3 ni mara mia nimchukue Godfrey Walusimbi kuliko Gadieli Michael....yeye (Gadieli) ni mzuri tu kwenye kushambulia....kitu ambacho Mohamed Husein Tshabalala anacho na zaidi

    ReplyDelete
  5. Hawa vijana wamedanganywa na washauri wabovu walionao kwa kudhani kuwa wana viwango vya juu ama kutafuta pesa nyingi kwa ajili ya maisha lakini wanashindwa kujua kuna siku utafilisika na pesa uliyopewa itaisha na itabidi utafute nyingine wakati huo kiwango kimeshuka hamna mtu aliye tayari kukusajili....na kwakuwa umri ni mdogo hata nje hawawezi kukuchukua ikiwa nidhamu yako n.a. kiwango chako kimeshuka.....pesa ni muhimu lakini sio kila kitu....wachezaji wetu inatakiwa wapewe somo la kujitambua ama sivyo wataishia humu humu kukata mitaa ya kariakoo

    ReplyDelete
  6. Hawa vijana wamedanganywa na washauri wabovu walionao kwa kudhani kuwa wana viwango vya juu ama kutafuta pesa nyingi kwa ajili ya maisha lakini wanashindwa kujua kuna siku utafilisika na pesa uliyopewa itaisha na itabidi utafute nyingine wakati huo kiwango kimeshuka hamna mtu aliye tayari kukusajili....na kwakuwa umri ni mdogo hata nje hawawezi kukuchukua ikiwa nidhamu yako na kiwango chako kimeshuka.....pesa ni muhimu lakini sio kila kitu....wachezaji wetu inatakiwa wapewe somo la kujitambua na uweledi, na namna ya kufikiria future yao zaidi katika kukuza na kuviendeleza vipaji vyao, ama sivyo wataishia humu humu kukata mitaa ya kariakoo

    ReplyDelete
  7. Simba haitaki ugomvi na mtu. Tazama hata wale waliokuwa wakaidi kuongeza mikataba pamoja na Okwi, Simba walikuwa wapole na huku wakiongea nao Kwa lugha ya Rehema na ya mapenzi. Haruna hakukubalisna na dau na Kwa Amani akaondoka na Okwi hata hii leo mazungumzo yakiendelea ikiwezekana Sawa haikuwezekana atakwenda Kwa Amani. Nani Simba hata mara moja iliwahi kupanic nae na huo ndio uungwana. Wale wachezaji Jonas Mkude na Ndelema si walianza mazungumzo na Yanga lakini je walikwenda? Through quiet diplomacy bila ya kupeana ultimatium wachezaji wakaamuwa kubaki. Neno Zuri lamtoa nyoka pangoni, walisema WA kale

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fuatilia historia ya Simba na Yanga utaona kuwa Yanga hawana utamaduni wa kubembeleza mtu.Mi nasema aende zake tu ikibidi namba tatu tutampanga hata Kindoki

      Delete
  8. Mpeni pesa anayoitaka mbona maneno mengi. Mkataba si imeisha sasa mbona mnatoa maelekezo kana kwamba ni mchezaji wenu bado. Muombeni hata bure anaweza kuja kuwachezeeni. Michango imeisha? Gaweni kadi Itisheni vikao vya Michango.

    ReplyDelete
  9. Lakin salehe uwe muungwana na siku zote, ukiwa muongo basi uwe uhakika wa kutunza kumbukumbu kuna habari ulitwambia za mwinyi zahera kuwambia viongozi wa Yanga wasimbembeleze Gadiel na ukasema hivi nakunukuu ulivyoandika ''Beki huyo kwa mara ya pili amegomea kusaini mkataba baada ya hivi karibuni kukataa dau la Shilingi Milioni 50 alilowekewa mezani huku Simba ikielezwa kumuwekea 70 ambazo ameshawishika kusaini miaka mitatu Msimbazi. lakin sasa unasema miaka miwili vip mjomba sisi tushakujua upo ukanda gani lakin usiwaunahau unapowadanganya watu.

    ReplyDelete
  10. kika mchezaji ana ndoto zake.
    ajibu alikuwa na ndoto za kuishia kucheza bongontu, ametaman hela zaid kuliko kutafuta mafanikio na kuuza jina.
    ni mchezaj gani ukanda wa A. mashariki anaeeza kukataa ofa ya mazembe na kubaki tz.
    aibu.
    ni kosa la kuwa na meneja kanjanja.
    hata kama simb wanakupa shi. milioni 2 zaidi ya mazembe, lkn huko ndipo wanatokea wnzake.
    hata huyu g. michael atulize akili kwanza.

    ReplyDelete
  11. Nashauri aachwe aende fedha sio kila

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawewe usiwe kama wasiofahamu michezo. Ukisema aachwe unakosea, wamuache kwani wa kwao?????
      Hapo wanamuomba kama walivyomuomba Litombo. Wasipomsajili inamaana TIMU imeshindwa sio imemuacha mchezaji

      Delete
  12. Lakini hata huyo Gadieli hamna kitu tuseme ule ukweli tu....magoli mengi hutokea kwake....Yanga mna bahati sana kwakuwa sasa mtaziba moja ya mapungufu ya beki mliyokuwa nayo msimu uliopita

    ReplyDelete
  13. Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic