AGGREY MORRIS AMPA KIBURI HIKI KOCHA AZAM
Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije ameingia kiburi cha kufanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwa na uhakika wa kurejea uwanjani nahodha wake, Aggrey Morris na kiungo Mudathir Yahya.
Wachezaji hao wawili wamekuwa nje kwa miezi kadhaa kutokana na kukumbwa na majeraha ya goti ambapo hawakuwepo katika kikosi hicho kwenye mechi za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema, Azam FC wakishinda kwa mabao 3-1.
Ndayiragije amesema kuwa anapata uhakika wa kufanya vizuri zaidi kwa kurejea kwa wachezaji hao wawili kutokana na msaada wao kwenye kikosi hicho.
Image result for Mudathir Yahya
“Kitu kizuri ni kuwa Aggrey na Mudathir wapo kwenye hatua za mwisho za kurejea kucheza na wenzao baada ya kuwa nje sababu ya majeraha.
“Hawa ni wachezaji wazuri na muhimu kwenye kikosi chetu, kuungana na wenzao kwa mara nyingine itatupa nafasi kubwa ya kutamba kwenye ligi lakini katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo tupo,” alisema Ndayiragije.
0 COMMENTS:
Post a Comment