NAHODHA wa timu ya KMC, Juma Kaseja amesema kuwa leo wanaanza kazi vema kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambayo inadhaminiwa na Vodacom.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa timu inatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu ila imejipanga kupata matokeo chanya.
"Ni mchezo wetu wa kwanza, tunaanza kete yetu tukiwa tupo sawa na tuna malengo ya kufanya vizuri, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti uwezo wa kufanya vizuri tunao," amesema.
Msimu uliopita KMC ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Azam FC, leo wanakutana tena uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu zote.
0 COMMENTS:
Post a Comment