August 14, 2019



AGOSTI 17 mwaka huu, Viwanja vya Mlimani City patakuwa hapatoshi kwani kutakuwa na uzinduzi wa mashindano Sprite Bball Kings msimu wa tatu.

Mashindano hayo maalumu kwa ajili ya mpira wa kikapu yanatarajiwa kuzishirikisha timu zaidi ya 52 kumtafuta bingwa mpya atakayepata zawadi ya shilingi Milioni 10.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Mradi  wa mashindano hayo, Janeth Bhoke amesema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuibua vipaji na yanajumuisha timu zote za kikapu ambazo zitajisajili.

“Timu zote za mpira wa kikapu ambazo zinajisajili kushiriki mashindano haya zitapewa ratiba kamili na kutakuwa na hatua mbalimbali mpaka kufikia hatua ya fainali, kikubwa ni kwa wachezaji kuwa na umri kuanzia miaka 16 na awe ni Mtanzania.

“Mshindi wa kwanza atapatiwa zawadi ya shilingi milioni 10 na kombe, mshindi wa pili atapewa zawadi ya shilingi milioni tatu na mchezaji bora wa mashindano atapata milioni mbili na kikombe chake,” amesema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic