UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na kupoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya
Fasil Kenema ya Ethiopia nafasi ya kusonga mbeke bado ipo.
Azam FC
mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 wana
kibarua kizito cha kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumbani unaotarajiwa
kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamazi.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa
kwa sasa kikosi kipo kambini na kinajiaanda na mchezo wake wa marudio.
“Tumepoteza
mchezo wa kwanza hatujapoteza matumaini naona tuna nafasi ya kusonga mbele
ukizingatia tutakuwa nyumbani.
“Ushindani
kimataifa ni mkubwa, wamepata ushindi mzuri kwao si mbaya kwetu tutatumia
uwanja wetu wa nyumbani kumaliza kazi na kusonga mbele kwenye michuano ya
Kimataifa,” amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment