UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao wa kesho dhidi ya Fasil Kenema
ya Ethiopia utakaochezwa kesho uwanja wa Bahir Dar.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa
tayari kikosi kimeanza kuyazoea mazingira nchini Ethiopia.
“Kikosi
kimewahi mapema nchini Ethiopia na tayari Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije
ameandaa program maalumu kwa ajili ya wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo
wetu.
“Mashabiki
watupe sapoti kwani tunajua kwamba tuna kazi ngumu ugenini hasa ukizingatia
michuano hii ya kimataifa ni hatua ya mtoano tupo tayari, imani yetu tutaonyesha ushindani mkubwa” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment