August 10, 2019



LEO Uwanja wa Taifa kutakuwa na kazi kubwa moja kwa mabingwa wa kihistoria Yanga kucheza mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ukiwa ni mchezo wa awali.

Yanga inapeperusha Bendera ya Taifa baada ya Tanzania kuongezewa timu shiriki kwenye michuano ya kimataifa wanaanza hatua ya awali kucheza na Rollers ya Botswana.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mara ya mwisho Yanga kushirki michuano ya kimataifa ilikuwa msimu wa mwaka 2018 baada ya kutwaa ubingwa wao mara msimu wa 2016/17 na walitolewa hatua za awali na Township Rollers.

Kwenye mchezo huo walipocheza na Township Rollers mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kabla ya kulazimisha sare tasa mchezo wa marudio Botswana.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema  kuwa wanawatambua vema wapinzani wao kwani waliwatoa walipokutana nao kwa sasa lazima wapambane kuweka rekodi mpya.

“Tunawatambua vema Township Rollers kwa kuwa walitutoa kwenye michuano wakati tulipokutana nao, kwa sasa hatukubali hilo tunataka tuweke rekodi mpya ya kuvuka hatua hii na kufika mbali zaidi,” amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic