August 15, 2019


NDEGE ya abiria ya Urusi  leo, Agosti 15, 2019, imeanguka baada ya ndege (mnyama) kuingia ndani ya injini na kusababisha mlipuko wa moto katika injini  hiyo huko Moscow.

Ndege hiyo ambayo ni Airbus 321 iliyokuwa na abiria 234 pamoja na wahudumu saba ilikuwa ikitoka Urusi kuelekea Simferopol na kulazimika kutua kwa dharura karibu na uwanja wa kimataifa wa Zhukovsky kusini-mashariki mwa Moscow.

Ndege hiyo iliyoangukia katika shamba la mahindi imesababisha Watu 55 kujeruhiwa wakiwemo watoto 17 wenye umri kati ya miaka miwili  hadi tisa, ambao wote wapo hospitali kwa matibabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic