August 20, 2019


Na George Mganga

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema nafasi ya usemaji ndani ya klabu hiyo ipo chini yake mpaka sasa.

Manara ameamua kuliweka wazi hilo kutokana na uwepo wa taarifa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari kuwa ataondoka kwenye nafasi hiyo.

Takribani wiki moja sasa imekuwa ikielezwa kuwa Mwandishi Gift Macha ambaye amekuwa akifanya kazi Azam Media anatajwa kuchukua nafasi ya Manara.

"Naomba ifahamike kuwa nafasi hii ipo chini yangu mpaka sasa.

"Siwezi kukaa Simba milele kwa kuwa hii ni klabu kubwa na yoyote anayefanya kazi hapa lazima ataondoka.

"Hii ni taasisi, ni kubwa kuliko mtu, si mimiwala si Crescentius Magori, wote tutaondoka".


2 COMMENTS:

  1. Kwa kuna shida gani anapashwa kutuambia kuwa bado analipwa mshahara kama mwanzo lakini swala la msemaji kisheria kwa sasa hana. Anaendelea kulipwa kwa kukusanya watu hapa imeshindikana jina la cheo chake tu. Ongera Simba kwa kujali watumishi

    ReplyDelete
  2. Wewe ni nani ambaye unajua kuliko bodi ya wakurugenzi ya Simba?Unajua hata mshahara wake?Mkataba wake?Watu wengine kwa kujijaza ujinga hawajambo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic