UONGOZI wa
JKT Tanzania umesema kuwa kwa sasa kazi imepamba moto kuelekea msimu mpya wa
Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu.
JKT Tanzania
kwa sasa imejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi na mchezo wao
wa kwanza utakuwa dhidi ya Simba Agosti
23.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Mohamed Abdalah ‘Bares’
amesema kuwa kikosi kipo vema.
“Kikosi kipo
salama na maandalizi yapo sawa kwa kuwa tupo sehemu tulivu mafuzo yanakaa kwenye
vichwa vya wachezaji kwa umakini mkubwa.
“Kila
mchezaji ana morali kubwa na matarajio yetu kurejea Bara itakuwa kati ya Agosti
20, mashabiki watupe sapoti kwani tunajua mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa
mgumu ila tupo tayari,” anesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment