FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa bado hajajua wachezaji wa Yanga ambao hawajajiunga na kikosi watarejea lini kwa sasa.
Juma Abdul na Andrew Vincent 'Dante' hawakujiunga na kikosi kambini Morogoro hata timu ilipojichimbia Visiwani Zanzibar hawakugusa kambini kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa wanadai stahiki zao.
Habari zinaeleza kuwa beki kisiki, Kelvin Yodani yeye amejiunga na timu ila sharti lake ni moja kama ilivyo wa wenzake kwamba ni lazima alipwe stahiki zake zote.
Mwakalebela amesema kuwa:"Kwa sasa sijajua wachezaji hao watarejea lini kambini kwa kuwa wao ndio walianza kugoma,
"Ni wachezaji muhimu na mchango wao ni mkubwa kama ambavyo walipambana msimu uliopita ila kwa sasa uongozi tutakaa ili kumaliza matatizo haya," amesema.
Kuna haja ya kuchunguza mambo ndani ya Klabu ya Yanga tatizo liko wapi? Nani ni kiini cha tatizo? Na jitihada zipi zimechukuliwa na Uongozi kutatua tatizo mpaka hivi sasa? Uongozi unafanya nini? Hili ni "doa" kwa Uongozi mpya....au Kuna mbinu chafu na hujuma kutoka kwenye mtandao mkubwa wa maadui wa Yanga walio ndani na nje na wenye nguvu serikalini.......Wanayanga sasa ni wakati wa kuamka na kunusuru hali hii!!!
ReplyDeleteSidhani kama kuna hujuma.Sio siri kwani wachezaji hawo wameweka hadharani malalamiko yao.Viongozi wanakubali kuwa hawajawalipa stahiki zao.Nafikiri nimewaelewa hawa wachezaji wamegoma baada ya kuona wachezaji wageni wakisajiliwa na kupewa stahiki zao wanapomalizana kusaini miktaba.Kivipi viongozi washindwe kuwapa stahiki zao hawo kina Dante, Yondani na Abdul hata kama pengine walikuwa hawahitaji....kulikoni? Tatizo kama ni hujuma unavyodai basi wa kuanza kumyoshea kidole ni kocha Zahera aliyedai hawezi kusajili mchezaji mzawa zaidi ya 30m na hapo tayari anajenga matabaka na hii itakuja kuwa-cost kama si leo basi mbeleni.Maana kuna fununu kuwa Dante na Juma Abdul wangetolewa kwa mkopo na Dante akakazia kusepa mazima hivyo akitaka kulipwa stahiki zake zote.Inashangaza kwa nini viongozi wasimalizane na hawo wachezaji ili waendelee na majukumu yao au ndio mwendo wa staili ile ile ya Ben kakolanya? Ndio kuhujumiana ?
DeleteKwa kweli hovyo kabisa kwa uongozi wa Yanga na wale wote wadau wanaojifanya kutaka kuirejeshea Yanga upya .kwanini Simba wasiwe juu? Simba walikuwa wawazi kwa wachezaji wasiokubaliana nao walimalizana na kuwapatia stahiki zao mapema wakasepa kabla ya kusajili wachezaji wapya. Tunawaomba viongozi wa Yanga waache kuwanyanyasa watanzania katika ardhi yao kwa kuona wageni ndio wenye stahiki yakusaminiwa kuliko wazawa.Tunaiomba serikali kuingilia kati suala la wachezaji wa Yanga wenye madai yao. Suala la wachezaji wa Yanga wenye madai yao kama lingekuwa suala la Simba vyombo vya habari vyote vingeandika habari za kuikashifu Simba.Hicho chama kinachojifanya watetezi wa haki za wachezaji wanachokitetea ni kitu gani? La kusikitisha pia hawa ni wachezaji muhimu kwa Yanga pia wakati Yanga ipo kwenye majukumu ya kuliwakilisha Taifa . Nakumbuka mechi iliyopita kati ya Simba na Yanga jinsi Dante alivyopambana na kuweza kuisaidia Yanga kuepukana na kipigo cha aibu.Chonde chonde wanayanga na wadau wa mpira ifanyike jitihada ya kutatua madai ya hawa wachezaji kwani hii ni aibu kwenye tasnia ya soka letu.
ReplyDeleteHata ligi haijaanza mishahara hakuna,ikianza ligi mtasema mnahujumiwa.Viongozi ndio wanahujumu timu.lipeni stahiki zao msije mkasingizia watani wanawahujumu
ReplyDelete