JULIANA Shonza, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ameongoza msafara ulioipokea timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' ambayo imerejea leo ikitoka Afrika Kusini ilikoalikwa kushiriki michuano ya COSAFA na imerejea ikiwa imebeba kombe hilo.
Mabingwa hao wa kombe la COSAFA wapo chini ya Kocha Mkuu, Bakari Shime wamepokelewa pia na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukiongozwa na Rais, Wallace Karia, pamoja na Katibu Mkuu, Wilfred Kidao.
Shime amesema kuwa shukrani kubwa ni kwa Mungu pamoja na TFF kwa kuwekeza kwa watoto.
"Tumejitoa na wachezaji wamecheza kwa juhudi pamoja na maandalizi ya muda mrefu, mbali na kombe tuna tuzo ambazo tumepokea ikiwa ni pamoja na ile ya mchezaji bora wa mechi ambapo tumebeba tuzo tatu, mchezaji bora wa mashindano hivyo inamaanisha kwamba tulikuwa vizuri," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment