August 10, 2019




UONGOZI Kagera Sugar, umesema kuwa kwa sasa upo tayari kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu ujao kutokana na maandalizi ambayo wanaendelea kuyafanya.

Kagera Sugar, ambao msimu uliopita waliweka rekodi ya kutwaa pointi zote sita kwa Simba wameweka kambi mkoani Kagera wakiendelea kujipanga kwa ajili ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani wa msimu ujao.

“Kikosi kimejipanga vizuri na kila mchezaji ana morali kubwa ya kuona tunafikia malengo yetu msimu ujao.

“Kwa sasa tunaendelea kucheza michezo ya kirafiki ili kupata kikosi bora, tumeanza na Singida United, Gwambina FC  na Mwadui FC hivyo bado tunaendelea kujipanga,” amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic