JACKSON
Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wa
marudiano wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
KMC
inapeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itacheza
mchezo wa marudio dhidi ya AS Kigali Agosti 23 baada ya kutoka suluhu ya bila
kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Rwanda.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo sawa na
wamejipanga kutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo.
“Makosa
ambayo tuliyafanya ugenini tumeyafanyia kazi, kwa sasa kikosi kipo tayari
kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wetu AS Kigali, mashabiki watupe
sapoti.
“Kwa sasa ni
wachezaji wachache ambao hawapo fiti ikiwa ni pamoja na Salim Aiyee, Ramadhan
Kapela, Charlse Ilanfia, James Msuva na Cliff Buyoya ambaye ameanza mazoezi
mepesi,” amesema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment