August 28, 2019


FULL TIME: Na mpira umekwiiiisha, Yanga wanalala bao 1-0 Uwanja wa Taifa.
Dak ya 90+5, Mussa anapiga shuti kali langoni mwa Yanga na kipa Shikalo anaupangua mpira, inakuwa kona.
Dak ya 90+4, Ruvu wanapata kona nyingine tena
Dak ya 90+3, Ruvu wanapata kona, dakika zimesalia mbili.
Dak ya 90+2, Ruvu wamefikisha kadi za njano tano, hukuwa Yanga wakiwa hawana hata moja, ni baada ya Said Dilunga kupewa kadi nyingine.
Dak ya 90+1, Lamine Moro anakosa nafasi nzuri akitengenezewa na Tshishimbi.
Dak ya 90, dakika 90 zimemalizika, dakika tano za ziada zinaongezwa.

Dak ya 89, Yanga wanapasiana nje ya eneo la 18 mwa Ruvu, lakini imekuwa ngumu kupenya ngome yao.
Dak ya 88, zimesalia dakika mbili mpira kumalizika.
Dak ya 86, Yanga wanapata kona, piga Ngassa lakini Ruvu wanaokoa.
Dak ya 85, Moses Shaban analimwa kadi ya njano, ni kadi ya nne kwa Ruvu.
Dak ya 84, Ruvu wamejaa langoni mwao, ni mbinu ya kuumaliza mchezo wakiwa na bao hilo moja bila majibu.

Dak ya 79, ni faulo imetokea, faida kwa Yanga, wanaanza harakaharaka kusaka bao la kusawazisha
Dak ya 79, kona nyingine kwa Yanga
Dak ya 77, hali bado ngumu kwa Yanga, wanahaha kusaka bao la kusawazisha.
Dak ya 75, Toto na mpira kati mwa uwanja, ni faulo, Ngassa aliyeingia kipindi cha pili anafanywa madhambi.
Dak ya 74, mpira unarushwa kuelekezwa Yanga, ni baada ya mchezaji wa Ruvu kuutoa nje kushoto mwa Uwanja.

Dak ya 71, mpaka sasa Ruvu wameshapatiwa kadi tatu za njano na Yanga hawana hata moja.
Dak ya 71, Kona nyingine wanapata Yanga, wakati huo Ruvu wanafanya mabadiliko.
Dak ya 70, Tshishimbiiii, piga tena shuti kali lakini kipa Hussein anaokoa, inakuwa kona, inapigwa lakini inaokolewa na mabeki.

Dak ya 69, Moro sasa anakwenda mbele, anapiga krosi lakini inaokolewa, Ruvu wameshaanza kujaa nyuma kulinda goli
Dak ya 68, Tshishimbi anapiga shuti kali nje ya 18 lakini linapaa juu ya lango, ni goli kiki.
Dak ya 67, Kalengo anatoa mpira nje baada ya kubabatizana na mchezaji wa Ruvu Shooting, unarushwa kuelekezwa Yanga.
Dak ya 66, Mwanachama wa Yanga, Abbas Tarimba yupo ndani ya Uwanja wa Uhuru akishuhudia mpaka dakika hii Yanga ikiwa nyuma kwa bao 1-0
Dak ya 66, Yanga wanarusha kwa haraka baada ya Ruvu kuto mpira nje, wanataka kusawazisha bao.

Dak ya 64, Yanga wanapata kona, anapiga Sibomana lakini inakuwa gaina mafanikio, inatoka nje, ni goli kiki.
Dak ya 63, Yanga wamefanya mabadiliko, ameingia Maybin Kalengo na Sandney Urikhob ametoka.
Dak ya 60, Said Dilunga ameumia, amelala chini na Machela imengizwa ndani kumbeba.
Dak ya 59, Kabamba Tshishimbi na gozi, mabeki Ruvu wanaokoa kwa kupiga mpira mbele kuelekea langoni mwa Yanga.
Dak ya 58, Toto anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea Ruvu.

Dak ya 57, Edward Christopher anatoka upande wa Ruvu na nafasi yake inachukuliwa na Abdereheman Mussa.
Dak ya 56, hatari katika lango la Ruvu, Balama na mpira kulia mwa uwanja, anapiga krosi lakini mabeki wa Ruvu wanaokoa.
Dak ya 55, kipa Bidii Hussein anaokoa shuti jingine kali la Yanga.
Dak ya 53, ngoma ni nzito kwa Yanga, bado wanapambana kusaka bao la kusawazisha, mpira ni goli kiki, unapigwa kueleka Yanga.

Dak ya Dak ya 52, Yanga wanafanya mabdiliko, Mapinduzi Balama anaingia kuchukua nafasi ya Juma Balinya.
Dak ya 51, Ruvu wanapoteana kati mwa Uwanja, ilikuwa ni nafasi nzuri kwao kutengeneza bao la pili.
Dak ya 50, Molinga mtu mzito na miguvu yake anaukokota mpira, sasa unarushwa kuelekea Yanga.
Dak ya 49, mpira wanao Yanga, Balinya, kwake Tshishimbi,  anagawa kwake Toto
Dakika 45 za kipindi cha pili zimeanza

Dakika 45 za kwanza zimemalizika

Dak ya 45, Molingaaa, piga kichwa lakini anakosa yeye na lango.
Dak ya 44, nahodha wa Ruvu anaumia, kabebwa nje kwa kutolewa na machela, faulo kuelekea Yanga, inapigwa lakini Ruvu wanacheza faulo.
Dak ya 43, anapiga Juma Balinya anapiga lakini mpira unapaa juu ya lango.
Dak ya 42, zimesalia dakika tatu pekee kwenda mapumziko, ni faulo kuelekea Yanga, Molinga anachezewa madhambi.

Dak ya 40, Ruvu Shooting wananamiliki mpira sasa kwenda mbele langoni mwa Yanga, wanajichanganya na inakuwa goli kiki.
Dak ya 39, Shikalo na mpira sasa langoni kwake, piga mbele huku unakwenda nje na Ruvu wanarusha kuelekea Yanga.
Dak ya 38, Mpaka sasa Yanga wameotea mara mbili na Ruvu mara moja.
Dak ya 37, kona nyingine wanapata Yanga, piga huku Sibomana lakini kipa anaokoa maridadi kabisa.
Dak ya 36, Yanga bado wanapambana kusawazisha, lakini Ruvu wameimalisha vizuri lango lao la ulinzi.

Dak ya 33, Mfungaji wa bao la Ruvu amelala chini, machela inambeba kumpeleka nje.
Dak ya 32, Molingaaaa, piga kule lakini kipa wa Ruvu, Bidii Hussein anaokoa, lilikuwa ni shambulio hatari.
Dak ya 31, Yanga wanapata kona, Sibomana anapiga lakini unaokolewa.
Dak ya 30, Yanga wanapambana kusaka bao la kusawazisha, mashabiki waliojitokeza ni kiwango cha wastani.
Dak ya 28, kipa wa Ruvu Shooting amelala chini, mpira umesimama kwa muda, anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda.
Dak ya 27, Tshishimbi anapiga heda moja kali lakini mpira uanshindwa kulenga lango.


Dak ya 23, mpira kwake Tshishimbi, pasia kwake Toto, Toto anampa Moro, inakuwa offside, Molinga anaotea.
Dak ya 20, Ruvu wanapiga mbele, kwenda mbele kwake Sadat Mohammed, piga pale anamvisha kanzu Shikalo, gooooooli, anafunga bao la kwanza
Dak ya 19, Ruvu wanapasiana eneo la langoni mwao, wanatoa nje.
Dak ya 18, Sibomana anachezewa faulo, inapigwa kuelekea Ruvu.
Dak ya 18, Shaban Msala anachukua mpira, inakuwa ni kona kuelekea Yanga, inapigwa lakini inaokolewa.

Dak ya 17, Tshishimbi tena kwake Sibomana, lakini anacheza ndivyo sivyo kwa Mtui, Ruvu wameshaanza.
Dak ya 16, Toto sasa na mpira, anapasia kwake Tshishimbi, Baraka Mtui anauchukua.
Dak ya 16, Tshishimbi amefanyiwa mazambi, mpira unapigwa kuelekea Ruvu.
Dak ya 15, Sibomana amepiga tena kona lakini na unamkuta Tshishimbi ambaye amepiga kichwa na mpira umeenda nje.

Dak ya 14, mchezaji wa Ruvu amelala chini, mwamuzi kasimamisha mpira

Dak ya 13, Yanga wanapata kona, anaenda kupiga Sibomana, amepiga lakini kipa anatoa nje na inakuwa kona nyingine.
Dak ya 11, faulo inapigwa lakini mabeki Yanga wanaokoa.
Dak ya 11, Molinga anacheza faulo, mpira unapigwa kuelekea Yanga.
Dak ya 10, Juma anapata nafasi ya kupiga shuti la kufunga nje ya 18, lakini linakosa makali, kipa Ruvu anadaka.
Dak ya 7, Yanga wana presha kubwa ya kusaka bao la kwanza, wakati huo Nahodha wa Ruvu, yupo chini akiwa ameumia.

Dak ya 5, Tshishimbi anafanya shambulio jingine kali, mabeki Ruvu wanaokoa.
Dak ya 4, Ruvu wanafanya shambulio la kwanza kwa Yanga lakini Shikalo anadaka.
Dak ya 3, Ruvu Shooting wanaunyaka, piga mbele langoni mwa Yanga,  Tshishimbi anaokoa na kutoa nje.
Dak ya 3, Mpira anao kipa Farouk Shikhalo, anapiga kuelekea mbele langoni mwa Ruvu.
Dak ya 1, mechi imenza kwa Yanga kufanya shambulio kali, lakini Sadney Urikhob anashindwa kumalizia pasi ya David Molinga.

Zimesalia dakika chache kwa mechi hii kuanza, kuwa nasi hapa kwa UPDATES zote.

8 COMMENTS:

  1. Dah kwani ubao unasomekaje?..mbona mapema hivi....Wacha nikalale

    ReplyDelete
  2. Hakuna timu hapo na hayo madira ya manjano nindeni kwenye ngoma mpira hamuwezi mnabebwa hadi dk 95 aibu yenu hiyo mazee hayo hovyooooo

    ReplyDelete
  3. Wavaa madira hao wamebebwa na refa dk 95 mazee hayoooooo

    ReplyDelete
  4. Hakuna timu hapo na hayo madira ya manjano nindeni kwenye ngoma mpira hamuwezi mnabebwa hadi dk 95 aibu yenu hiyo mazee hayo hovyooooo

    ReplyDelete
  5. Siku njema huonekana asubuhi na hiyo ndio asubuhi yenu na huku mkijipanga kukomba makombe yote pamoja like la Afrika. Chaliiiii. Wamepoteza furaha ya kuondolewa Mnyam

    ReplyDelete
  6. Balinya Oyee, Faruku Oyee, GSM mimins hela tubebe makombe yote

    ReplyDelete
  7. Hivi kuna siku yoyote Huyu kocha ameshawahi kufungwa na kukubali kuzidiwa bila ya visingizio hata kama wakati mwingine anapokuwa yuko sahihi....mimi binafsi sikumbuki siku aliyohojiwa na kukubali kufungwa kutokana na kuzidiwa kimbinu na kiufundi sikumbuki. Yanga kuweni makini sana msipelekwepelekwe!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic