August 28, 2019


Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa Yanga kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa timu hizo mbili.

Bao pekee na Ruvu Shooting limewekwa kimiani na Sadat Mohammed akimvisha kanzu kipa Farouk Shikalo mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza.

Bao hilo limeweza kudumu kwa dakika zote 90 mpaka Mwamuzi Martin Saanya alipohitimisha mchezo wa kupuliza kipyenga cha mwisho, ubao ukisomeka 1-0.

Katika mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera aliwatoa wachezaji Sadney Urikhob na kumwingiza Maybin Kalengo, Juma Balinya akimtoa pia na nafasi yake akichukua Balama Mapinduzi lakini mabadiliko hayakuleta mafanikio.

Ruvu imeweka rekodi kwa mara ya kwanza kufuta uteja kwa Yanga tena ikiibuka mshindi ikiwa ugenini.

Kama mdau wa michezo, unaweza kutuambia Yanga waliteleza wapi? Ndondosha maoni yako hapo chini.


5 COMMENTS:

  1. Tatizo la muunganiko wa forwardline ya timu bado ni kubwa....utengenezaji wa nafasi ni mkubwa lakini umaliziaji ni tatizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1. Hawakuwa na nidhamu ya ukabaji
      :
      2. wachezaji walikuwa wanashambulia zaidi kuliko kulinda

      Delete
  2. Kwani lazime washinde Ruvu nao walijipanga

    ReplyDelete
  3. Nasema kocha kachemka kuiunganisha safu ya ushambuliaji kwani inakosa utulivu wachezaji wanapiga mashuti kama watoto. Kama kocha hawezi kurekebisha safu hiyo kuna sehemu ya timu itaumia. Makali ya forward hufanya timu isishambuliwe sana, kiungo huimalika sana.

    ReplyDelete
  4. zahera amesema kuwa Yanga haikupaswa cheza mpira wa leo eti kwa kuwa walikuwa Dar? Inaonekana hicho alichokuwa anapiga kelele msimu uliopita eti kwa nini Simba hawafanyi, hadi ikafikia simba inacheza mechi kila baada ya siku 48 leo kasahau..Sio kwamba TFF hawakupokea barua ya kuahirisha mechi, bali walijua wasingebadilisha sababu Yanga na Zahera walilalamika sana msimu uliuopita

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic