August 26, 2019


Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amefunguka kuwa wala hakuwa na presha wakati Yanga ilipokuwa ikikipiga dhidi ya Township Rollers kwa kuwa alijua mapema lazima angeshind amchezo huo.

Nchemba ambaye ni mlezi wa Singida United, lakini pia inafahamika ni mwanachama na mshabiki mkubwa wa Klabu ya Yanga ambapo kwa nyakati tofauti amekuwa akitangaza kuisaidia Yanga kusajili wachezaji.

Akizungumzia ushindi wa juzi wa bao 1-0 ambapo Yanga walikuwa ugenini, Nchemba alisema alijua Yanga watashinda kwa kuwa kocha amefanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji ambao kwa kiwango fulani wameonyesha uwezo mkubwa wa kuipa mafanikio timu.

“Naipongeza timu yangu kwa kupata ushindi na kusonga hatua inayofuata nilijua mapema kuwa tutapata ushindi kwa sababu ya mabadiliko kadhaa yaliyofanywa msimu huu, katika mchezo ule wameonyesha utofauti kati ya wanaume na vijana,” alisema Nchemb

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic