August 26, 2019


Straika wa Yanga, Juma Balinya, juzi alimwagiwa noti za maana na mashabiki wa timu hiyo wanaoishi Bostwana.

Fedha hizo zilitokana na kufunga bao muhimu ambalo liliipa nafasi Yanga ya kuendelea kusalia kunako Ligi ya Mabingwa Afrika.

Balinya aliifungia Yanga bao mnamo dakika ya 42 katika mechi ambayo ilimalizika kwa ushindi wa 1-0 na kuiwezesha kukutana na Zesco United katika mchezo utakaofuata.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, amethibitisha ni kweli Balinya alipokea fedha hizo kutoka kwa mashabiki.

Aidha, Msolla, ameeleza kuwa wamepanga kuwapa fedha wachezaji wote waliokuwa kwenye msafara kama motisha na yote hii inachagizwa na ushindi wa juzi.

1 COMMENTS:

  1. jaman msiwajaze saaana sifa baado hata hawajaanza kazi, kwa hyo angalieni msije mkawapotosha sana na habari zetu pia mashabiki kuweni wavumilivu msijaze kichwani kuwa sasa wamefika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic