August 30, 2019


SIMBA wikiendi iliyopita iliondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada kutoka sare ya bao 1-1 na UD do Songo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Matokeo haya yamewafanya Simba kuondolewa kutokana na sheria ya bao la ugenini baada ya sare ya 0-0 ugenini. Simba wameondoka baada ya msimu uliopita kufika kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, wakiwa na rekodi ya kushinda michezo yote ya mtoano nyumbani.

Hata hivyo kuna mambo mengi ambayo yalichangia timu hiyo kuondolewa, viongozi wa timu hiyo ni kati ya watu ambao wanahusika moja kwa moja kwenye adha hii ambayo imewakuta mashabiki lukuki wa timu hiyo ambao walikuwa wamejazana uwanjani:

HAKUNA MBADALA WA BOCCO

Simba walifanya usajili mzuri kwa ajili ya michuano hiyo, lakini moja ya jambo ambalo walionyesha kuwa walikuwa hawajajiandaa nalo ni kwamba kuna siku watamkosa mshambuliaji wao, John Bocco. Kukosekana kwa mshambuliaji huyo kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita kulionyesha kuwa Simba walikuwa wanamtegemea Meddie Kagere pekee na baada ya yeye kukabwa hawakuwa na njia nyingine.


Fedha zilizotumika kuwasajili Wabrazil watatu ambao hawajaisaidia timu hiyo na wamekuwa wakiishia benchi na jukwaani, zilikuwa zinaweza kuisaidia Simba kumpa mshambuliaji mmoja mahiri sana hapa Afrika au zilikuwa zinaweza kuwafanya Simba wakampa Okwi fedha alizokuwa anataka ili abaki kwenye timu hiyo na labda angeweza kuwasaidia.

KUJIAMINI SANA

Pamoja na kwamba Simba walikuwa wanatakiwa kucheza michezo hii miwili ya hatua ya awali ili wapate nafasi ya kwenda kwenye hatua inayofuata, lakini waliona kama vile siyo kitu sana.

Viongozi wa Simba walikuwa wanazungumza zaidi kuhusu kufika nusu fainali badala ya kuamini kuwa wanatakiwa kupenya kwanza kwa UD do Songo ndiyo wafike huko. Hii imeonyesha kuwa hawakuutilia mkazo sana mchezo huu ndiyo maana hata kutolewa kwao kumewafanya hata wenyewe washangae.

MATOKEO YA MSIMU ULIOPITA

Msimu uliopita Simba walifanikiwa kushinda michezo yote nyumbani kwao na walikuwa wanafungwa idadi kubwa ya mabao ugenini. Hii iliwafanya waamini kuwa itakuwa ni kazi rahisi zaidi kupata ushindi tena nyumbani baada ya kutoka sare ugenini.

Hii iliendelea kuwapa kiburi hata matangazo ya mara kwa mara ambayo walikuwa wakiyatoa msimu uliopita kuwataka mashabiki kwenda uwanjani hawakuyatoa kwa wingi kwenye mchezo huu wakiamini kuwa mashabiki watajaa tu kwa kuwa ni mazoea.

KIKOSI KIDOGO: Kocha wa Simba hakuwa na kikosi kipana cha kutosha kucheza mchezo mkubwa
kama huu na kilimsumbua hata kupanga.

Hii inaonyesha kuwa kikosi ambacho kocha huyo alikianzisha uwanjani hakikuwa na mbadala nje ndiyo maana hakukuwa na wachezaji bora kwenye benchi ukiachana na Hassan Dilunga.

Kitendo cha Patrick Aussems kumtoa Francis Kahata na nafasi yake kuchukuliwa na Dilunga kabla ya dakika 45 za kwanza kumalizika, kilionyesha kuwa tayari kocha huyo ameshaona tatizo.

Kutokana na uhaba wa wachezaji wa kushambulia kwenye timu hiyo ndiyo maana kocha huyo aliamua kumuingiza Miraji Athuman ambaye anaonekana kabisa hakuwa kwenye mipango yake.

Lakini pia kwa kuwa kocha alikuwa anatafuta mabao na hana jinsi akajikuta akimtoa Gadiel Michael na nafasi yake kuchukuliwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambao wote ni mabeki wa pembeni. Kwa kocha ambaye ana wachezaji wengi kuanzia dakika ya sabini alikuwa anaweza kumtoa beki yeyote na kumuingiza mshambuliaji kwa kuwa ni muda wa kutafuta mabao zaidi kuliko kulinda.

9 COMMENTS:

  1. Analysis ya kijinga Simba ilifungwa kutokana na ubovu wa beki na baada ya kupata bao Songo wakaamua kufa kujilinda wakijua hawana cha kupoteza.

    ReplyDelete
  2. Simba haijawahi kuaibika isipokuwa ilifikia pahala ambapo timu yoyote haijawahi kupafikia. Ikiwa Simba imeaibika utaielezea vipi Ile timu iliyofungwa katika mchezo wake WA mwanzo na timu ambayo dhaifu inayofungwafungwa na vitimu visivokuwa na viwango

    ReplyDelete
  3. Kweli mchambuzi huna akili, simba iliziba mapengo yote, salamba - wilker da silva, kotei-shiboub, niyonzima-kahata, okwi-kanda/miraji athumani/Ajibu. Kilichotokea siku ya mechi ni ukosefu wa bahati au umakini katika kufunga magoli, mashambulizi yalikuwa mengi ya kutosha, mbadala wa Bocco angeweza kuwa wilker au Ajibu ila bahati mbaya ni majeruhi, ila mchambuzi unaposema kuwa hakuna mbadala wa Bocco nauona ufupi wako wa uelewa na kuongea kwa mahaba

    ReplyDelete
  4. nakuunga mkono Simba walipoteza umakini kwani walikosa nafasi nyingi za wazi halafu naona umewakomalia sana wabrazil Simba ndio wanajua kwanini wamewasajili subiri baada ya miezi9 sita ndio uongee

    ReplyDelete
  5. kama simba imetoka wiki mbili zimepita sasa lakini bado tu e jaman si ninyi mfanye vyema mliobaki mnatuchosha bwana a wabrazil, kwani mlichangia sh ngapi mbona kuna watu wamesajili maghalasha weeengi lakini hatusemi?, acheni hata klabu kubwa ulaya zinatolewa bwana msituchoshe PSG iliwahi kupigwa 6 na ikiwa na mtaji mkubwa sana, mbona kuna habari nyiiingi za kuandika mpaka simba tuuuu ebo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanatuchosha kwa kweli na hawa wachambuzi vilaza.Simba imefanya usajili mzuri na wa kuridhisha.Watu wamewakomalia Okwi,Kotei na Niyonzima as If hawakuwepo tulipokuwa tunapoteza mechi za ugenini kwa kufungwa kwa aibu.Walisaidiaje? Msitake kuwaalaumu sana viongozi wakati pengine nao walijitahidi kuwabakisha hawo wachezaji lkn huenda walitaka dau la kukomoa kama ulivyoona kwa Okwi ambaye kwa tamaa zake ilishindikana kujiunga na tinu ya falme za kiarabu kwa kuweka dau lisilo fikirika kichwani.Wakati mwingine maisha yaendelee na hakuna faida ya kuangalia nyuma.Zamaleki, Orlando Pirates zimetolewa raundi ya kwanza na ni vilabu tajiri na venye wachezaji mahiri wanatoka Amerika ya kusini iweje mnaikomalia Simba? Simba ilikosa umakini wa kufunga magoli licha ya kutengeneza nafasi nyingi na kuupiga mwingi sana.FIFA/CAF watuondelee hizi sheria zao zilizopitwa na wakati wa goli la ugenini linahesibika mbili.Bora ya penalties.

      Delete
  6. Naona analysis nyingi zinatoka magazetini. Kilichosaidia Simba kufika robo fainali ni pamoja na kubadilika kwa calendar ya CAF. Mechi za CL zilianza September wakati ligi ilishaanza kwahio timu ilikuwa tayari kwa mashindano. Mwaka huu timu imecheza mechi za kirafiki hazizidi kumi na baadhi ya wachezaji hawajacheza bado. Timu inahitaji muda na kilichotokea msimu huu ni part of the learning process. Simba ni project kubwa huwezi kusajili chap chap ukapata mafanikio hapo hapo. Marekebisho yataendelea kuwepo ila focus itakuwa ni kubeba kombe. Watu watakosa outings za kwenda uwanjani kwaajili ya mechi za CL ila ni kwa muda to na ndio timu kubwa zinavyojengwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic