VAN DIJK AWABWAGA MESSI NA RONALDO
Enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni, na usiku huu beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk amewaangusha.
Van Dijk amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 Van Dijk baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita.
Kama Luka Modric alivyofanikiwa kuwaoondoa Ronaldo na Messi katika udhibiti wa tuzo hiyo mwaka jana - Van Dijk amekuwa mtu wa pili kuwapiku nyota hao ambao wametamba kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.\
Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southampton na amekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji la Ligi ya Premia dhidi ya Manchester City hadi mwisho.
Kabla ya leo alikuwa hajawahi kutwaa tuzo kubwa yeyote. Lakini usiku huu analala na tuzo mbili; mchezaji bora wa Ulaya na beki bora wa Ulaya.
Takwimu za michezo ya mwaka 2018-19 zinaonesha kuwa Van Dijk aliiwakilisha klabu na taifa lake katika mechi 59.
Alifunga mabao tisa na kusaidia ufungaji wa mabao manne. Pia alichezea Liverpool kwa dakika nyingi zaidi ya mchezaji mwingine yeyote (4,465) .
Katika mashindano yote ameonesha kwa zaidi ya 70% umuhimu wake kama beki.
Liverpool ilifungwa mabao machache(22) ikilinganishwa na vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita na Van Dijk alichangia ufanisi huo kwa 76.3%.
Ukimlinganisha Van Dijk na mabeki wengine wa Ligi tano kubwa Ulaya mchezaji huyo aliongoza katika msimu wa 2018-19 kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo.
0 COMMENTS:
Post a Comment