August 21, 2019



UONGOZI wa KMC inayoshiriki michuano ya Kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho umeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya kubashiri ya M-bet wenye thamani ya bilioni moja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja Masoko wa M-bet, Allen Mushi amesema kuwa wameamua kuichagua KMC kati ya timu 20 ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara kutokana na mafanikio ambayo wameyapata kwa muda mfupi.

“M-bet tumeichagua KMC kutokana na namna ambavyo imejipambanua vema katika sekta ya mpira baada ya kupanda daraja ilikuwa ikifanya vema na imeleta ushindani mkubwa.

Mwenyekiti wa bodi ya KMC, Benjamini Sitta amesema  kuwa,: "M-bet ni kampuni maalumu ya michezo ya kubashiri na tumeingia nao mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya bilioni moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic