August 21, 2019


ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba Mganda, Emmanuel Okwi ambaye amesajiliwa na klabu ya Al Ittihad ya Misri msimu huu hatashiriki michuano ya kimataifa akiwa na klabu yake hiyo mpya.

Hii ina maana kuwa wachezaji wapya wa Simba msimu huu akiwemo Sharaf Shiboub, atakuwa amemfunika Okwi kwa kuwa yeye amecheza michezo hiyo ya kimataifa tofauti na Mganda.

Nyota huyo amesajiliwa kwa muda wa miaka miwili na ametambulishwa rasmi katika klabu hiyo juzi wakiwa kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Okwi alisajiliwa na klabu hiyo baada ya mkataba wake na Simba kumalizika na klabu moja kutoka Falme za Kiarabu ilikuwa ikimuhitaji nyota huyo lakini ilishindwa ndipo Rais wa Al Ittihad, Mohamed Mosselhi, alimaliza mchezo na kuingia naye mkataba mpaka mwaka 2021.

Kwa misimu miwili mfululizo akiwa na klabu ya Simba, Okwi alifanikiwa kushiriki michuano ile ya Kombe la Shirikisho ambapo waliishia raundi ya pili kwa msimu wa 2017/18 baada ya kutolewa na Al Masry ya Misri.

Nyota huyo akiwa na Simba msimu uliopita alipambana na kuweza kuisaidia timu yake kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilifika hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo.

Hivyo nyota huyo hataweza kutamba kimataifa msimu huu mpaka pale msimu ujao kama timu hiyo itafanya vyema kwenye mechi zake za ligi kuu. Msimu uliopita Al Ittihad ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi huku ikivuna alama 39 tu.

Hata hivyo, msimu mpya wa ligi unatarajiwa kuanza Oktoba mwaka huu na kumalizika mwezi Mei mwakani. Okwi amewahi kuichezea klabu ya Simba, Yanga, Etoile Du Sahel ya Tunisia, SönderjyskE na SC Villa ya Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic