August 14, 2019




PASCAL Wawa, beki wa Simba amesema kuwa mashabiki wasiwe na presha kuelekea mchezo wa marudiano wa kimataifa dhidi ya UD do Songo unaoatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Taifa.

Simba inapeperusha Bendera ya Taifa kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo mchezo wa kwanza wa awali wakiwa ugenini walilazimisha sare ya bila kufungana.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa mchezo wa marudio utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya kwa kuwa watakuwa nyumbani.

“Mechi za kimataifa zina ushindani wake na kila timu inahitaji kusonga mbele kwa sasa tunajipanga kurudiana nao nyumbani imani yetu tutapata matokeo mazuri.

“Kwa sasa hakuna haja ya kuwa na presha kubwa kwani makosa ambayo tuliyafanya mchezo wa kwanza yamefanyiwa kazi na tunawaomba mashabiki watupe sapoti,” amesema.

2 COMMENTS:

  1. na hasa makosa ya defence line. hatutegemei kuona tunafungwa magoli ya free headers, clearances zinazorudisha mpira ndani ya box na overconfidence ya kupiga chenga ndani ya eneo la hatari. Bado mapema sana lakini tahadhari ni muhimu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic