August 26, 2019


Mapambano ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati, yamefanyika kwa kishindo usiku wa kuamkia leo Agosti 24, 2019 Club 361 Mwenge jijini Dar es Salaam.


Mabondia wametifuana kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki huku wajeda nao wakijiwinda na michuano ngumi za ridhaa ya kimataifa ya majeshi yanayotarajiwa kufanyika mapema hivi karibuni.

Katika mtifuano huo mkanda wa Ubingwa Afrika Mashariki uzito wa Unyoya ulianza kupiganiwa na Issa Nampepechena Nassibu Ramadhani pambano lililokuwa na raundi kumi ambapo Nassibu aliibuka na ushindi.

Pambano lingine la Ubingwa wa Afrika Mashariki uzito wa Bantam nalo lilikuwa la raundi kumi kati ya bondia, Tonny Rashid na Haidari Mchanjo ambapo Tonny ndiye aliyeutwaa mkanda huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic