UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya mtoano dhidi ya Zesco utakaopigwa mwezi ujao kati ya Septemba 13-15.
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vema kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Msolla amesema kuwa kwa sasa mpira una mabadiliko makubwa na mipango mikubwa inawezekana.
"Tupo vizuri na tuna imani ya kufanya vema kimataifa, kwa sasa hatuna presha kwani hata tukitolewa kwenye hatua hii tuliyopo tutadondokea kombe la Shirikisho, tutaendelea kuwa kimataifa," amesema.
Yanga imerejea usiku wa kuamkia leo ikitokea nchini Botswana ikiwa na ushindi wa bao 1-0 na imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1.
Uongozi wa Yanga uitayarishe timu kwa mazoezi zaidi. Pia uhamikishe vibali kwa wale wachezaji wa kigeni vime patikana haraka.
ReplyDeletePia msemaji wa timu aendelee na kazi yake vizuri na asiwe msemaji ovyo au kubwatuka bwatuka ovyo kama wengine.
Sisi tunaiamini timu inawezo wa kusonga mbele zaidi.
YANGA IMARA.