MOHAMED Salah, mshambuliaji wa Liverpool anazidi kuwa mtamu ndani ya kikosi hicho huku akiendelee kuifukuzia rekodi ya kutetea kiatu chake cha ufungaji bora msimu huu wa mwaka 2019/20.
Salah kwa sasa ana jumla ya mabao matatu aliyopachika mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu England inayoendelea kunoga.
Kwenye mchezo wao wa Kwanza dhidi ya Norwich City iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 alitupia bao moja na kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Arsenal alitupia mabao 2.
Msimu uliopita alitupia jumla ya mabao 22 na kutwaa kiatu cha mfungaji bora akiwa na mshikaji wake wa Karibu, Sadio Mane pamoja na Pierre Aubameyang wa Arsenal.
Huu ni msimu wake wa tatu akiwa ndani ya Liverpool Arsenal hawana bahati naye kila wanapokutana uwanjani.
Kwenye jumla ya michezo mitano ambayo Salah amecheza na washika bunduki hao amewatungua jumla ya mabao Sita.
Amefanikiwa Kwa asilimia Mia kuiweka timu yake ndani ya sita bora ndani ya kikosi hicho ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ulaya pamoja na Super Cup.
0 COMMENTS:
Post a Comment