September 26, 2019


LEO Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoa wa Kagera, kapeti lake litawaka moto kuhimili mikikimikiki ya wanaume 21 watakaokuwa kazini kusisaka pointi tatu kwa udi na uvumba ndani ya dakika 90 za mchezo.

Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime leo itacheza mchezo wake wa kwanza ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kucheza jumla ya michezo mitatu ya ligi kwa msimu wa 2019/20 wakiwa ugenini.

Kete yao ya kwanza ilikuwa dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume na walishinda Kwa bao 1-0 na Yusuph Mhilu dakika ya 15.

Mchezo wao wa pili ilikuwa dhidi ya Alliance FC na ilishinda kwa mabao 2-1, mabao yao yalifungwa na Evarigitius Mujwahuki dk ya 20 na Yusuph Mhilu dakika ya 68

Mchezo wa tatu mambo yalizidi kunoga na waliibuka na Ushindi mbele ya Mbao FC uwanja wa Nyamagana lilipachikwa kimiani na Awesu Awesu dk ya 68 na mchezo wa tatu waliibuka na Ushindi wa bao 1-0 lilipachikwa na Awesu Awesu.

Kwa upande wa wageni Simba wao wamecheza jumla ya michezo miwili na wameshinda yote wakiwa wamejikusanyia jumla ya poiti sita zote ikiwa ni Uwanja wa nyumbani Uhuru kuanzia ule wa Kwanza dhidi ya JKT Tanzania Kwa Ushindi wa mabao 3-1 na ule wa pili ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar Kwa mabao 2-1.


Zote mblii zinalinda rekodi zao mpya

Timu zote mbili zimekuwa na mwanzo mzuri kwa msimu huu wa 2019/20 licha ya moja kuwa ugenini na moja kuwa nyumbani bado zimeonyesha zimeanza kipekee 

Kagera Sugar imeanza kwa kushinda mfulululizo ndani ya dakika 270 huku Simba ilishinda ndani ya dakika 180 hivyo makocha wote hesabu zao itakuwa ni kulinda rekodi zisitibuliwe mapena kabla ya ligi haijashika kasi.

Kisasi kwa Simba

Mechi ya leo itakuwa ni ya kulipa Kisasi Kwa kikosi cha Simba ambacho msimu uliopita walipoteza jumla ya pointi sita Kwa Kagera Sugar walianza kupoteza wakiwa ugenini kwa kufungwa mabao 2-1 kabla ya Vita Yao kumalizikia uwanja wa Uhuru na bao la Mohamed Hussein ndilo jina lake.

Wakati Simba ikipigia hesabu Kisasi, wao hesabu zao kufuta kumbukumbu ya kupoteza michezo mingi ya hivi karibuni dhidi ya Simba uwanja wa Kaitaba.

Tangu msimu wa mwaka 2014/15 mlaka msimu huu, Kagera Sugar imekutana na Simba mara tano na kushindwa kufurukuta kwenye mechi mbili ambazo ni msimu wa 2014/15, Simba iliinyoosha mabao 2-1, 2015/16.

Kagera ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mara ya mwisho kupoteza ilikamilika msimu wa 2017/18 Kagera ilifungwa bao 1-0 na Simba Jambo linalowatesa viongozi wa Kagera. Sugar hivyo utamu wa vita uanzidi kuongezeka.

Hawa hapa nyota watakaokosekana

Ni Simba pekee leo itawakosa nyota zake wawili ambao ni nahodha John Bocco na mlinda mlango Ally Salim ambaye yupo na Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 kwenye michuano ya CECAFA.

Nyota hawa wameshikilia ni wa kuchungwa

Matokeo ya timu kutokana na kutimiza majukumu Yao Kwa umakini, kwa upande wa wenyeji ni mshambuliaji Yusuph Mhilu ambaye ana mabao mawili huku Awesu Awesu akiwa nalo moja  bila kusahau kwamba kuna mashine ya kazi ambyo msimu uliopita alikuwa ni Super Sub alipokuwa Mbao Kwa sasa yupo na Kagera Sugar.
.Kwa upande wa Simba wao wanajovunia  uwepo wa Kagere ambaye ametupia jumla ya mabao 3 pamoja na Super Sub, Miraj Athuman ambaye amepachika mabao mawili na yote akitokea benchi.

Maingizo mapya kukutana leo

Kwa msimu huu, nyota hawa itakuwa nu mara yao ya Kwanza kumemyanana na Kagera Sugar wakiwa wamevaa jezi  zao Simba ambao ni Mbrazili Wilker sa Silva, Gerson Fraga, Tairone Santos, Francis Kahata, Deo Kanda, Sharaf Shiboub, Kennedy Juma, Beno Kakolanya, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael.

Kwa upande wa Kagera Sugar kuna mashine mpya kama mlinda mlango, Benedict Tinocco, Mwashiuya, Awesu Awesu, Yusuph Mhilu na Mujwahuki, Zawad Mauya.

Kosi la Kagera litakuwa namna hii

Said Kipao langoni, Gereza Mwita, David Luhende, Erick Kyaruzi, Zawad Mauya, Geoffrey Mwashiuya, Abdalah Seseme, Evarigitius Mujwahuki na Yusuph Mhilu..

Hili hapa jeshi la Simba

Aish Manula langoni, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ' Tshabalala', Erasto Nyoni,Tereone Santos, Gerson Fraga, Deo Kanda, Mzamiru Yassin, Sharaf Shiboub na  Meddie Kagere na 
Hassan Dilunga.

Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera alisema kuwa wanawatambua wapinzani zao wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa...
"Tupo tayari na tunambua kwamba mpira ni ndani ya Uwanja na sio propaganda ama jujivunia rekodi hakuna kitu kama hicho tunahitaji matokeo chanya hicho kingine," 

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba alisema kuwa bado Ligi Inaanza na mwendelezo wao wa kupata matokeo chanya bila wasiwasi ..

"Nimewaambia wachezaji wangu kuwa kwenye mechi zetu zote, tunahitaji pointi tatu muhimu kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ushindani nasi tunahitaji Ushindi,".

Imeandaliwa na Lunyamadzo Mlyuka

2 COMMENTS:

  1. Mwandishi hajui hata idadi ya wachezaji wa timu zote mbili.21??Kuna mmoja tayari keshapewa kadi nyekundu na mpira haujachezwa?.

    ReplyDelete
  2. Lets pray for our team.simba nguvu moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic