September 26, 2019


Baba Mzazi wa Mshambuliaji wa KR Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta ametuma maombi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kumpatia mtaa mtoto wake huyo kutokana na historia aliyoiweka katika soka la Tanzania kwa kuwa eneo hilo ndio chimbuko lake.

Samatta ambaye anakipiga Genk ameweka rekodi kadhaa katika soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mchezaji Bora Afrika akiwa na TP Mazembe pamoja na kucheza ligi ya Ubelgiji historia ambayo haijawekwa na mchezaji mwingine hapa nchini.

Mzee Samatta alisema kuwa; “Baada ya mheshimiwa Makonda kumpa Samatta mtaa hapa Dar, nimeonelea ni vyema kupeleka maombi kwa wakuu wa Wilaya ya Kibiti ili kuweza kumpa heshima na kujua chimbuko lake ni wapi, Samatta ni Mdengeleko halisi, mimi baba yake nimetokea huko Kibiti hivyo ni vyema kuweka ukumbusho.”

“Ingekuwa fahari kuona Mndengeleko kutoka Rufiji ndio amefanikiwa kuweka rekodi katika historia ya soka la nchi hii pia kuwafahamisha watu kujua Samatta ametokea wapi.

“Tayari nimeshatuma maombi hayo na yanafanyiwa kazi iwapo watakubaliana na ombi langu basi wakati wowote anaweza kupewa mtaa,” alisema Mzee Samatta.

1 COMMENTS:

  1. huyu mzee aisee duuu anapenda sifa sana utafikiri yeye ndio anacheza mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic