September 1, 2019


Alichokizungumza mchezaji Amri Kiemba kuhusiana na utofauti baina ya Simba na Yanga hiki hapa.

"Kuna mchezaji anastahili kucheza Yanga na kuna mchezaji anayestahili kucheza Simba kulingana na tamaduni za hivi vilabu viwili kwa sababu mimi nimecheza vilabu vyote viwili.

"Yanga wanacheza kupata matokeo, kwao haijalishi sana wamecheza vipi. Simba wanahitaji kupata matokeo na kucheza vizuri, kwa hiyo vilabu hivi vinahitaji wachezaji wa aina mbili tofauti.

"Mchezji anayecheza kwa kujitoa zaidi anaweza akadumu Yanga kuliko Simba na mchezaji mwenye udambwidambwi anaweza kupata sana nafasi Simba.

"Mchezaji kama James Kotei alikuwa anaonekana wakawaida tu Simba ukimlinganisha na wachezaji wengine labda watu wanaoangalia mpira kwa jicho jingine.

"Angalia mchezaji kama Chama, Niyonzima au Okwi walivyokuwa na majina makubwa Simba. Kotei angekuwa anacheza Yanga, angekuwa mchezaji mkubwa sana.

"Simba hata ikipoteza mchezo lakini ikacheza vizuri watu wataona ni bahati mbaya lakini mkishinda huku mmecheza vibaya watu bado watalalamika, kucheza mpira mzuri ni utamaduni wa Simba."

CHANZO: CLOUDS FM

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic