RATIBA SIMBA YAVUNJWA
Benchi la ufundi la timu ya Simba chini ya Kocha wake Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems, limevunja kambi ya mazoezi kwa muda wa siku tatu.
Maamuzi ya Aussems yamekuja kwa ajili ya kuwapa wachezaji mapumziko na Alhamis ya wiki hii wataendelea na ratiba hiyo.
Likizo hiyo fupi kwa wachezaji wa Simba inakuja kufuatia wiki hii kuwa inayohusisha mechi ya timu za taifa.
Simba itendelea kujinoa Alhamis hii kuendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment