September 10, 2019


RICHARD Djodi, kiungo mshambuliaji wa Azam Fc ameongeza mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi cha  mabosi hao wa Dar es Salaam.

Djodi amesaini mkataba huo mpya leo akiwa sambamba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'. Mkataba huo utamfanya kuendelea kusalia kwa wababe hao wa Azam Complex kwa miaka mitatu, hadi mwaka 2022.

Uongozi wa Azam FC umeamua kuingia naye mkataba mpya ndani ya muda mfupi, baada ya Djodi kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi mbalimbali za mashindano hali ambayo imemvutia Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, aliyependekeza kurefushwa zaidi kwa mkataba wake.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast amesajiliwa akitokea Ashanti Gold ya Ghana, ambapo hadi sasa katika mechi tatu za mashindano alizoichezea Azam FC amefunga mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic