ETIENNE
Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa anawapigia hesabu kali
wapinzani wake wa kimataifa ambao ni timu ya Triangel FC kutoka Zimbabwe.
Triangel imepenya hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuiondosha
Rukizno ya Burundi kwa jumla ya mabao 5-0 itamenyana na Azam FC iliyoiondosha
Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2, kati ya Septemba 13 -15.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije
amesema kuwa tayari ameona makosa yao yalipo na ameanza kuwapa program maalumu
vijana wake kwa ajili ya mchezo wake wa kimataifa.
“Nimegundu
makosa ya vijana wangu yalipo na uwezo wao pia, taratibu ninakuwa na kikosi
bora ambacho kitahimili mikikimikiki ya kimataifa nina imani ya kupata matokeo
chanya.
“Kwa kuwa
tutakuwa nyumbani ni wakati wa mashabiki kuendelea kutupa sapoti kama ambavyo
walifanya awali kwenye mchezo wetu dhidi ya Fasil Kenema,” amesema Ndayiragije.
0 COMMENTS:
Post a Comment