ABDALAH Panzi, maarufu kama 'Dulla Mbabe' leo amerejea ardhi ya Bongo na kupokelewa na umati wa mashabiki ambao walijitokeza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea.
Mbabe amerejea baada ya kumyoosha mpinzani wake kwa TKO Mchina, Zulipikaer Maimaitiali katika raundi ya tatu na kubeba ubingwa wa Super Middle wa WBO Asian Pacific.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mbabe amesema kuwa ni furaha kubwa kwake kupeperusha bendera ya Taifa na kurejea na ubingwa.
"Kwangu ni furaha kubwa kubeba ubingwa na kurejea nao katika ardhi ya Tanzania, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti yao kubwa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment