September 3, 2019



MSIBA kwa Taifa kwa timu za nyumbani kupoteza mapema kwenye michezo ya kimataifa hasa kutokana na matumaini na matarajio ya wengi kwa timu hizo zilikuwa na nafasi ya kufanya vizuri ukizingatia michezo yao ya mwisho wamecheza wakiwa nyumbani.

Matokeo ambayo wameyapata hayajawa ya kufurahisha machoni na maskioni mwa mashabiki jambo ambalo limewafanya wengi kubaki kimya wakiwa na maumivu yao moyoni.

 Wapo ambao walishindwa kujizuia kwa kulia na kushindwa kurejea nyumbani kutokana na kuhofia kuchekwa na majirani zao ambao waliwekeana miadi na imani kibao kwamba timu zao zinafanya kweli  uwanja wa nyumbani.

Kupoteza uwanja wa Taifa kwa Simba na KMC kwenye michuano ya kimataifa kiukweli ni pigo kwa mashabiki na wafuatiliaji wa mpira ndani na nje ya Bongo.

Matokeo ambayo Simba waliyapata ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na UD do Songo nyumbani hayajawa na faida kwa Simba zaidi ya kuwapa faida wageni kusonga mbele.

Pia matokeo ya mabao 2-1 waliyopata AS Kigali mbele ya KMC uwanja wa Taifa hayajawa na faidia kwa ndugu zetu KMC zaidi ya kuwapa nguvu jirani zetu AS Kigali kusonga mbele.

Haikuwa sehemu ya mipango ya mashabiki pamoja na timu mwisho wa siku haya ni matokeo baada ya dakika tisini kukamilika ndani ya uwanja.

Inaumiza  kwa jinsi inavyotokea tena kwenye ardhi ya nyumbani kwa timu kupoteza ikiwa na lundo la mashabiki ila hakuna namna ya kufanya zaidi ya kukubali kwamba  ni matokeo ya mpira.

Yanga, Azam FC na Malindi wanapaswa pongezi kwa kupata ushindi mnono kwenye michezo yao ambayo walicheza kwa kupata ushindi ambao kwa kiasi chake umewatoa kimasomaso mashabiki wengi wa mpira.

Jambo kubwa na la pekee ambalo linapaswa likae vichwani mwa mashabiki kwamba mpira ni ndani ya uwanja na sio nje ya uwanja huko tunafarijiana tu.

Msimamo niliuona kwa mashabi kiujumla unazidi kuleta picha nzuri hasa kwa kuwa na mshikamano kwenye mechi zote za kimataifa zilizochezwa.

Kuanzia ule wa kwanza wa Yanga kisha ukaja mchezo wa KMC, Azam FC mpaka wa Simba bado sapoti ya mashabiki imekuwa ikionekana dhahiri.

 Sapoti ya mashabiki imekuwa ikionekana waziwazi kwa kila timu bila kubagua na zile kasoro ambazo awali zilikuwepo ghafla zimeondoka na kumekuwa na umoja madhubuti kwa kila shabiki.

Hivyo ndivyo ambavyo inatakiwa kuwa kila siku hasa wakati wa mechi za kimataifa hatupaswi kufikiria uadui na kuleta utofauti wetu kwenye masuala ya kimataifa tutaushangaza ulimwengu mapema.

Matokeo ambayo yametokea uwanjani ni ya kuyapokea kwa mashabiki wote na kukubali kwamba tumekosea na tumepoteza hakuna njia nyingine ya kuweza kuyabadili.

Sapoti iendelee mwanzo mwisho kwa timu ambazo zimesonga hatua inayofuata ambazo ni Azam FC, Malindi na Yanga bila kujali ule ushabiki wa timu zetu ambazo tumekuwa tukizipenda na kuzishangilia mwanzo.

Azam imecheza, KMC. Malindi, Simba zote mashabiki wametoa sapoti tangu awali na inapaswa iendelee kwa timu zilizobaki kwa kuendelea kuonyesha moyo wa kuzipa sapoti bila kukoma.

Matokeo yanaumiza endapo mashabiki na viongozi bila kusahau wachezaji wakiendelea kuyafikiria kwa sasa kitu kimoja kinatakiwa kuyakubali yaliyotokea na kuruhusu maisha yaendelee.

Timu ambazo zinaendelea na mapambano zifanye kweli mbele ili kuendeleza furaha ya mashabiki na raha ya mashabiki wa Tanzania ambao wanapenda na kufuatilia mpira.

Tumeshindwa kusonga mbele kutokana na kanuni za mpira kutukataa haina maana kwamba hatuna uwezo wala hatukuwa na nia hapana matokeo yametukataa kwa baadhi ya timu nyingine zimepeta.

Haina tatizo kubwa kwani wakati ujao itakuwa ni fundisho kwa timu ambazo zimetolewa mapema hatua za awali kujipanga kufanya makubwa zikiwa kwenye michuano mikubwa ya Afrika.

Kila kitu kinawezekana iwapo waliopita kwenye michuano hii wakaanza maandalizi mapema na kujipa muda wa kufanya vizuri na kupata mbinu za kupata ushindi.

Hatua hizi za mwanzo zina ugumu wake kwani ukiteleza kidogo mwenzako anatokea hapohapo na kusonga mbele kimataifa na kukuacha ukizubaa hujui cha kufanya.

Maandalizi yaanze mapema kwa timu zetu kujipanga kupeperusha Bendera ya Taifa kwani hakuna tumaini jingine kwa timu kufanya vema zaidi ya hizi ambazo zimebaki.

Mashabiki wana imani na timu zao kimataifa na pia wanapenda kuona zinafanya vizuri sio kuishia hatua za awali itazidi kuwaumiza zaidi.

Wachezaji mna madeni makubwa kwa mashabiki na mnapaswa muyalipe kwa vitendo hasa mkiwa uwanjani kwa kucheza kwa ushirikiano mkubwa na nidhamu isiyo ya kawaida.

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Vita dhidi ya Yanga si ndogo....sasa tusubiri reaction ya wapenzi wa soka wa timu ya wananchi ....vurugu yake si haba ....itajengengeka dhana kuwa sheria na kanuni ziliundwa zikiwa na kusudio kwa mlengwa wa adhabu....Kuongoza Soka kwa chuki si "afya" kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania....mapungufu ya kiutendaji na kiutawala yanapoainishwa na kusemwa inakuwa makosa....uhuru wa kukosoa na kutoa maoni ni uhuru wa kikatiba ambao kila mtu anao uhuru huu usikandamizwe kwa kutunga kanuni na sheria...ili kuzuia watu kukosoa mapungufu yanayotokea katika uendeshaji na usimamizi wa tasnia ya mchezo wa soka hapa Tanzania.

    USHAURI
    Yanga msitoke nje ya reli jiandaeni na Zesco mashabiki waujaze uwanja wa Taifa..ili muudhihirishie umma Yanga ni baba lao

    Ahsante

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic