AZAM FC kwa sasa ipo nchini Zimbabwe ikiendelea kuivutia kasi timu ya Triangel United itakayoskutana nayo uwanjani Septemba 28.
Jeshi la Azam FC kwa sasa linapiga tizo mara mbili kwa siku ambapo asubuhi ya leo zoezi hilo lilikamilika pia zoezi la pili ni muda wa jioni kwa lengo la kuyazoea mazingira ya huko.
Tayari, Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije ameanza kuwapa mafunzo vijana wake ili kumaliza ngwe ya pili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya Kwanza.
Ndayiragije amesema kuwa ana matumaini na kikosi chake kupata matokeo chanya kutokana na mbinu ambazo anawapa kwa sasa ili kusonga mbele.
Azam FC inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Chamazi.
All the best
ReplyDeleteAzam na yanga nawatakia kila la kher ktk mashindano, mfuzu hatua ijayo.
ReplyDelete