September 27, 2019


Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA imekumbwa na shutuma nzito juu ya kura zilizomchagua Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kushinda tuzo hiyo ikidaiwa kura zilikuwa za uongo.

Katika hatua nyingine Bodi inayoratibu tuzo hizo imesema kura za Nchi ya Misri hazikuhesabiwa kwasababu saini zilikuwa zimeandikwa kwa herufi kubwa.

FIFA imeeleza hayo baada ya Chama cha Soka cha Misri kutaka kujua ni kwanini kura ya Kocha wa timu yao ya Taifa, Shawki Ghareeb na nahodha Ahmed hazikuhesabiwa.

Aidha, Kocha wa timu ya Sudan, Zdravko Logarusic na nahodha wa Nicaragua, Juan Barrera wamedai kupitia Mitandao ya Kijamii kuwa kura zao zilizoeneshwa na FIFA hadharani hazikuakisi machaguo yao.

Lugorisic amedai kuwa chaguo lake la kwanza lilikuwa Mshambuliaji wa Misri, Mohammed Salah lakini FIFA imeonesha chaguo lake ni Messi huku Barrera naye akidai kutompigia kura Messi kama FIFA ilivyodai.

3 COMMENTS:

  1. Inashangaza kabisa kwani Mesi alishindwa kuiwezesha Argentina kufanya chochote cha maana.Barcelona ilipigwa kipigo cha aibu na Liverpool na kutupwa nje ya UEFA champions league na Mesi ndani,wakati Ronaldo akiwezesha Portugal kubeba ubingwa wa ulaya nakadhalika.Hii ya Mesi mara hii FIFA wamechemka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani ilikuwa inamtaja mchezaji bora au timu yenye mafanikio? Acheni ushamba ni messi pekee ndie mchezaji alifikisha malengo ya soka kwa kiwango.

      Delete
    2. Sababu za kufunga magoli au asst kisiwe kigezo pekee cha kumtunuku mchezaji . Kama ni hivyo makipa na mabeki nilini watakuwa wachezaji bora . Jina la hii tuzo mimi nashauri iitwe tuzo ya wafungaji bora , na zianzishwe tuzo 3 nyingine za mabeki bora/makipa bora/viungo bora

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic