UONGOZI wa Mbeya City umesema kuwa umejipanga kufanya makubwa msimu huu kutokana na ushindani uliopo ndani ya ligi.
Mbeya City ilikuwa na mchezo Septemba 18 dhidi ya Yanga ambao umeondolewa na utapangiwa tarehe nyingine.
Sababu za kuuondoa mchezo huo umetajwa kuwa ni kuipa nafasi
timu ya Yanga kujiaandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Zesco
nchini Zambia.
Juma Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa timu ipo tayari kwa ajili ya ushindani wa ligi kuu msimu huu na itafanya maajabu.
Mchezo wa kwanza waliocheza Mbeya City ililazimisha sare dhidi ya Tanzania Prisons.
0 COMMENTS:
Post a Comment