September 4, 2019


Ukame wa mabao aliouonesha mshambuliaji Mnamibia wa Yanga, Sadney Urikhob katika mechi za mashindano yote ikiwemo za kirafiki, umemuibuka aliyekuwa straika wa timu hiyo, Mrundi, Amis Tambwe, kwa kusema anahitaji kupewa muda ili kufanya vema.

Tambwe amefunguka juu ya mshambuliaji huyo anayevaa namba 17 aliyokuwa akiitumia wakati anawatumikia mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara mara 27, akisema Urikhob ni mgeni na hajazoea mazingira hivyo hapaswi kuhukumiwa wakati huu.

Mpaka sasa Urikhob amefunga jumla ya mabao mawili pekee katika jumla ya mechi 14 ambazo Yanga wamecheza, mechi hizo zinajumuisha zile za kirafiki, Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Urikhob alifunga mabao hayo mawili katika mechi za kirafiki zilizochwezwa mjini Morogoro zilizokuwa sehemu ya maandalizi ya kucheza na Township Rollers kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu Bara.

"Urikhob bado ni mchezaji mgeni ambaye hajazoea mazingira ya Tanzania, anahitaji muda ili afanya vizuri.

"Mbali na ugeni wa mazingira, Urikhob pia ni mgeni pia ndani ya kikosi cha Yanga, hivyo suala la kuanza kumjadili mapema si sahihi kwa sababu huu ni mpira na huwa unahitaji muda kuendana na mfumo haswa pale unapokuwa umehamia timu tofauti na uliyoizoea.

"Najua ni kazi kubwa kutenegeneza rekodi kama yangu, ila akipambana na kujituma vizuri anaweza"akafanya vema," alisema Tambwe.

Katika msimu wa 2013/14, Tambwe akiwa na jezi namba 17 alifanikiwa kuibuka kuibuka mfungaji bora kwa kuingia kambani mara 19 akiwa Simba na baada ya kutua Yanga msimu wa 2015/16, Tambwe alikuwa mfungaji bora kwa kupachika jumla ya mabao 21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic